Umoja wa Afrika wasisitiza tena mshikamano wa Afrika kwa watu wa Palestina

(CRI Online) Desemba 01, 2023

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Faki Mahamat amesisitiza tena mshikamano wa Afrika kwa watu wa Palestina.

Mwenyekiti huyo amesema hayo katika taarifa iliyotolewa Jumatano katika hafla ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na Watu wa Palestina.

Bw. Faki amesema siku hiyo ya kimataifa ya mshikamano na watu wa Palestina inayoadhimishwa kila mwaka Novemba 29, ni siku ya kusisitiza tena jumuiya ya kimataifa kuendelea kufanya juhudi kuunga mkono harakati ya haki ya uhuru na uundaji taifa kwa Palestina.

Bw. Faki amesema, maadhimisho hayo ya watu wa Palestina ni ya dharura sana. Matukio ya uhasama yanayoendelea katika ukanda wa Gaza na kukaliwa kwa ardhi, ni ukiukwaji dhahiri wa sheria ya kimataifa na sheria ya kibinadamu ya kimataifa, ambao umeleta athari kwa maisha ya raia wa Palestina na kwa amani katika kanda hiyo kwa ujumla.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha