Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa pili wa AfCFTA kuhusu Wanawake katika Biashara

(CRI Online) Desemba 01, 2023

Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania, Dk Ashatu Kijaji amesema Tanzania itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa pili wa Eneo la Biashara Huria la Afrika (AfCFTA) kuhusu wanawake na biashara wenye kaulimbiu isemayo “Kuimarisha Ushiriki wa Wanawake katika Biashara na Kuharakisha Utekelezaji wa AfCFTA”.

Akizungumzia mkutano huo kwenye mkutano na waandishi wa habari Novemba 29, 2023, Kijaji amesema umeandaliwa na wizara hiyo kwa kushirikiana na Sekretarieti ya AfCFTA.

Kuhusu hatua iliyopigwa Tanzania katika kutekeleza sehemu ya makubaliano ya AfCFTA, waziri huyo amesema kuwa, Serikali ya Tanzania imeshakamilisha maandalizi ya Rasimu ya Itifaki ya Wanawake na Vijana katika Biashara ndani ya Makubaliano ya Eneo la Biashara Huria la Afrika (AfCFTA).

Amesema, itifaki hiyo sasa inasubiri kuidhinishwa na mawaziri wa biashara wa AfCTA ili kuanza kutumika mwaka 2023/24.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha