Mji wa Shenzhen, China: Mchanganyiko unaoendana vema wa usasa, jadi na mazingira asilia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 04, 2023

Ukiwa ni mji kubwa mwenye kiini cha mji kilichochangamana, shughuli nyingi za kiuchumi, na maendeleo makubwa, Mji wa Shenzhen nchini China unatilia maanani maendeleo yake ya kijani na uhifadhi wa ikolojia mijini. Kwa uwazi, mji huo unatoa umuhimu sawa katika uhifadhi wa ikolojia na maendeleo ya uchumi, ukiendelea kutafuta njia zenye uvumbuzi za maendeleo endelevu.

Bustani ya Yunhai na Bustani ya Ufukwe wa Dameisha ni sehemu ya mkusanyiko wa maeneo ya kiikolojia katika Wilaya ya Yantian mjini Shenzhen, yanayotofautishwa na milima na sifa zake maalum za bahari. Baada ya kukamilika kwa mradi wa kurejesha ikolojia kwa pande zote katika Bustani ya Ufukwe wa Dameisha, mandhari ya mji mwenye mimea ya aina mbalimbali imeleta taswira mpya. Bustani ya Yunhai inapatikana katika eneo la msingi la Bustani ya Yantian Banshan ambayo inaenea kwenye eneo lenye ukubwa wa kilomita zaidi ya 69.5. Eneo lote la msitu linajulikana kwa kuwa na utoaji mkubwa wa oksijeni. Na ni lenye ayoni hasi kwa wingi. Kwa hivyo, wikiendi na siku za kazi, wapiga kambi, waendesha baiskeli, na watalii wengi hutembelea bustani hiyo ambayo ni maarufu sana mtandaoni.

Kadri tunapoendelea kuzunguka katika kujionea sehemu mbalimbali za Shenzhen, nina shauku ya kuona namna Shenzhen inavyotumia kanuni ya kwamba "maji safi na milima ya kijani ni mali." Jiunge nami katika video hii ili kujionea hali ya kipekee ya kuendana kwa mazingira ya ikolojia ya Shenzhen!

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha