Mradi wa kulinda mito ya barafu wazinduliwa kwenye Banda la China la Mkutano wa Tabianchi wa COP28

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 04, 2023

Picha hii iliyopigwa kutoka angani Juni 16, 2023 ikionyesha mandhari ya Mto Baishui wa Mito ya Barafu Namba 1 kwenye Mlima wa theluji wa Yulong ulioko katika Mji wa Lijiang, Mkoa wa Yunnan, Kusini-Magharibi mwa China. (Xinhua/Chen Xinbo)

Picha hii iliyopigwa kutoka angani Juni 16, 2023 ikionyesha mandhari ya Mto wa Barafu Namba 1 wa Mto Baishui kwenye Mlima wa theluji wa Yulong ulioko katika Mji wa Lijiang, Mkoa wa Yunnan, Kusini-Magharibi mwa China. (Xinhua/Chen Xinbo)

DUBAI - Mpango wa kulinda mito ya barafu duniani umezinduliwa siku ya Jumapili kwenye Banda la China la Mkutano wa 28 wa Nchi Watia Saini wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) mjini Dubai, Falme za Kiarabu.

Kwenye shughuli hiyo ya mkutano wa COP28, watu wa ujumbe mbalimbali na wanasayansi walitoa maoni yao juu ya hatari za kuyeyuka kwa mito ya barafu na njia za kupunguza mchakato huo.

Watu wakipiga picha mbele ya banda la China kwenye Eneo la Kijani la Mkutano wa 28 wa Nchi Watia Saini wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28), mjini Dubai, Falme za Kiarabu, Desemba 3, 2023. (Xinhua/Wang Dongzhen)

Watu wakipiga picha mbele ya banda la China kwenye Eneo la Kijani la Mkutano wa 28 wa Nchi Watia Saini wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) mjini Dubai, Falme za Kiarabu, Desemba 3, 2023. (Xinhua/Wang Dongzhen)

Mradi huo uliopewa jina la “Kumbukumbu za Mito ya Barafu: Mpango wa Ufuatiliaji Duniani" umezinduliwa ili kuimarisha utafiti na ulinzi wa mito ya barafu na pia kuongeza ufahamu wa umma.

“Mito ya Barafu inabeba ushuhuda wa historia ya mabadiliko ya tabianchi kwenye sayari ya Dunia, na kuyeyuka kwa mito ya barafu kutaleta hatari mfululizo mbali na kuinuka kwa viwango vya bahari,” washiriki kutoka ujumbe mbalimbali wamesema.

Wameongeza kuwa, hatari zinazoweza kujitokea zitajumuisha uharibifu wa mazingira ya milima mirefu, ongezeko la hatari za maporomoko ya ardhi na mafuriko, pamoja na upotezaji wa shughuli za utalii na mali za kitamaduni.

Hatua zinazohitajika kuchukuliwa ni pamoja na kupunguza hali ya joto kuongezeka duniani kupitia kupunguza utoaji wa hewa chafu na kuimarisha mikakati ya uhimilivu inayoweza kusaidia kupunguza athari za hatari. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha