Timu ya Madaktari wa China visiwani Zanzibar waendesha kliniki za bila malipo kwenye Kiwanja cha Ndege cha Abeid Amani Karume

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 06, 2023

Kundi la 33 la timu ya madaktari wa China wanaotoa msaada kwa Zanzibar limetoa huduma za bila malipo za kliniki za afya tarehe 3 na 4 kwenye Kiwanja cha Kimataifa cha Ndege cha Abeid Amani Karume cha Zanzibar, Tanzania.

Kliniki hiyo ya bila malipo, imetoa huduma ya upimaji wa afya na mashauriano ya kitabibu kwa wahudumu zaidi ya 400 wa kiwanja hicho, na kutoa mpango wa matibabu na dawa za bila malipo.

Ofisa wa Wizara ya Afya ya Zanzibar Salim Slim akiwa kwenye kliniki hiyo ameishukuru timu ya madaktari hao wa China kwa kutoa msaada wa tiba kwa watu wa Zanzibar katika miaka 59 iliyopita, na kueleza matumaini yake ya kuimarishwa kwa uhusiano zaidi na timu hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa kiwanja hicho Rob William amesema kuwa, madaktari wa China ni marafiki wazuri wa Zanzibar, na huduma hiyo ya bila malipo ya kliniki imesaidia sana wahudumu wa kiwanja hicho cha ndege na kulinda afya zao.

Kiongozi wa kundi hilo la madaktari Jiang Guoqing amesema kuwa, kuwahudumia watu wa Zanzibar ni lengo la wakati wote la kundi hilo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha