Rais wa China akutana na viongozi wa Umoja wa Ulaya

(CRI Online) Desemba 07, 2023

(Picha inatoka Shirika la Habari la China Xinhua.)

(Picha inatoka Shirika la Habari la China Xinhua)

Rais Xi Jinping wa China leo Alhamisi mjini Beijing amekutana na Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel na Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen ambao wako nchini China kuhudhuria mkutano wa 24 wa viongozi wa China na Umoja wa Ulaya.

Rais Xi amesema, tangu mwishoni mwa mwaka jana baada ya ziara ya viongozi hao wa Umoja wa Ulaya nchini China, uhusiano kati ya China na Ulaya umeonesha mweleko mzuri wa maendeleo, hali inayoendana na maslahi na matarajio ya watu wa pande mbili. Amesema, China na Ulaya zinapaswa kufanya juhudi kwa pamoja ili kudumisha mwelekeo huo mzuri.

Rais Xi ameainisha kuwa, huu ni mwaka wa 20 tangu China na Ulaya zianzishe Uhusiano wa Wenzi wa Kimkakati wa Pande Zote. Amesema China na Ulaya zinapaswa kuendelea kuongeza kiwango cha kuaminiana kisiasa, kujenga maafikiano ya pamoja ya kimkakati, kuimarisha uhusiano wenye maslahi ya pamoja, na kupanua mazungumzo na ushirikiano, ili kunufaisha watu wa pande hizo mbili.

Pia amesema China na Ulaya zinatakiwa kukabiliana kwa pamoja na changamoto zinazokabili dunia, na kushirikiana katika kuhimiza utulivu na ustawi wa dunia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha