Shenzhen, China: Mji wenye utamaduni anuai na ulio wazi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 07, 2023

Shenzhen ni alama muhimu ya sera ya mageuzi na kufungua mlango ya China. Kwa zaidi ya miaka 40, mji huo umepitia mageuzi makubwa kutoka kuwa kijiji cha wavuvi kilicho mbali na kuwa mji wa kisasa wa kimataifa. Ukiendeshwa na uvumbuzi wa kisayansi na maendeleo yenye ubora wa juu, Shenzhen inaonyesha haiba yake kupitia utamaduni wenye nguvu na anuai, ikiunganisha China na Dunia.

Shenzhen ina maeneo mengi ya alama ya kihistoria na kitamaduni. Mji wa Gankeng Hakka, ambao zamani ulikuwa makazi ya watu wa Jamii ya Hakka, umehifadhi vichochoro na majengo wa kale, ukijichanganya vilivyo na milima inayozunguka.

Ngome ya Dapeng, ngome ya kijeshi kutoka Enzi za Ming (1368-1644) na Qing (1644-1911) za China ya Kale ni moja kati ya miji ya kijeshi iliyohifadhiwa vizuri ya China kuanzia Enzi ya Ming nchini China, na iliorodheshwa kwenye kundi la tano la maeneo muhimu ya Taifa ya mabaki ya kitamaduni yanayolindwa.

Maendeleo ya kisasa ya Shenzhen yanatoa uzoefu wa kitamaduni uliochangamana. Bandari ya Luohu, ambayo ni njia muhimu kwa wasafiri kati ya Shenzhen na Hong Kong, ina mchango mkubwa katika kuunganisha miji hii jirani. Mji huo pia unajulikana kwa "Mtaa wa Kwanza wa kufungua mlango wa biashara ya China" na Jumba la Makumbusho ya Sanaa la Shenzhen lenye mambo ya Kidijitali, ambalo linaonyesha mchanganyiko wa teknolojia na sanaa.

"Kuna mitindo mingi tofauti, na watu wengi tofauti. Ni tofauti sana. Ni pana sana. Siyo tu yenye taswira moja, lakini ni pana sana," amesema Esther Philander, mwimbaji wa Afrika Kusini.

Shenzhen ni mji jumuishi na wenye kukumbatia wahamiaji, hali ambayo hutoa aina mbalimbali za mila, ladha na sanaa, zikiungana katika mazingira ya kipekee ya mji huo. Moyo wa mji huo umeonyeshwa kwenye msemo, "Unakuwa mtu wa Shenzhen mara tu unapokuja hapa."

Huku ikihifadhi kwa bidii tamaduni zake anuai, Shenzhen inakaribisha watu kutoka kote China na duniani kote. Mji huu unaostawi unachangia mafanikio yake, ukiruhusu wageni kupata wakati mzuri wa mtindo wa maisha ya mji huo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha