Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi afanya mazungumzo na mwenzake wa Angola Tete Antonio

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 07, 2023

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC),  akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola Tete Antonio mjini Beijing, China, Desemba 6, 2023. (Xinhua/Yan Yan)

Beijing - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amefanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola Tete Antonio mjini Beijing siku ya Jumatano ambapo amesema chini ya mwongozo wa kimkakati wa wakuu wa nchi hizo mbili, uhusiano kati ya China na Angola umedumisha mwelekeo wenye nguvu wa maendeleo, na kupata matokeo mengi mazuri ya ushirikiano wa kufuata hali halisi, hali ambayo imeleta manufaa yanayoonekana kwa watu wa pande hizo mbili, na kutoa msukumo muhimu kwa maendeleo ya Angola na kuweka mfano kwa ushirikiano wa Kusini-Kusini.

“China ingependa kunufaika pamoja na Angola na uzoefu wake wa maendeleo na fursa katika soko la China, kupanua ushirikiano wa kufuata hali halisi katika miundombinu, uchumi wa kidijitali, nishati safi, huduma za afya na usalama wa chakula, kuimarisha mawasiliano kati ya watu, na kuimarisha zaidi msingi wa Urafiki wa China na Angola,” amesema Wang, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC).

Ameeleza nia ya China ya kuimarisha uratibu kwenye majukwaa ya pande nyingi na Angola, kuendeleza utaratibu wa ujenzi wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), kujenga jumuiya ya karibu zaidi ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja, kulinda kwa pamoja haki na maslahi halali ya nchi zinazoendelea na kuhimiza maendeleo ya utaratibu wa kimataifa katika mwelekeo wa haki na halali zaidi.

Kwa upande wake Antonio amesema kuwa Angola itafuata kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja na kuiunga mkono China katika kulinda mamlaka ya nchi na ukamilifu wa aridhi.

Antonio amesema, “Ushirikiano wa pande mbili za China na Angola una manufaa kwa pande zote”, Angola inakaribisha uwekezaji wa China, na iko tayari kuendelea na mawasiliano na uratibu wa karibu na China. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola Tete Antonio mjini Beijing, China, Desemba 6, 2023. (Xinhua/Yan Yan)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha