Mkutano wa mawaziri wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wafunguliwa nchini Ghana ili kuimarisha amani duniani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 07, 2023

Wajumbe wakiwa katika picha ya pamoja kwenye Mkutano wa Mawaziri wa Kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa wa Mwaka 2023 mjini Accra, Ghana, Desemba 6, 2023. (Picha na Seth/Xinhua)

Wajumbe wakiwa katika picha ya pamoja kwenye Mkutano wa Mawaziri wa Kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa wa Mwaka 2023 mjini Accra, Ghana, Desemba 6, 2023. (Picha na Seth/Xinhua)

ACCRA - Mkutano wa Mawaziri wa Kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa wa Mwaka 2023 ambao unakusanya wajumbe zaidi ya 600, wakiwemo mawaziri wa ulinzi na mambo ya nje, na maafisa maandamizi wa serikali na wa kijeshi umefunguliwa mjini Accra, Ghana siku ya Jumatano ili kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazokabili ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa na kufanya kazi kuelekea matokeo madhubuti ili kuimarisha ufanisi wa operesheni za kulinda amani duniani kote.

"Mkutano wa mwaka huu unafanyika wakati muhimu. Ulinzi wa amani, chombo cha ubunifu na chenye nguvu zaidi cha Umoja wa Mataifa ambacho kimeleta amani na utulivu katika maeneo mengi duniani, ikiwa ni pamoja na Bara la Afrika, kinakabiliwa na changamoto mpya," amesema Makamu Rais wa Ghana Mahamudu Bawumia katika hotuba yake ya ufunguzi.

Amewakumbusha wajumbe umuhimu wa kuwa na mtazamo thabiti wa kuzuia migogoro, ikiwa ni pamoja na hatua zinazosaidia kushughulikia vyanzo vya migogoro vinavyoathiri utulivu wa jamii yoyote ya binadamu.

Amesisitiza haja ya kutafuta na kupunguza mapengo katika ulinzi wa amani, kutathmini machaguo kwa ajili ya mabadiliko yenye maana, na kufanya kazi kuelekea matokeo halisi ili kuimarisha ufanisi wa shughuli za ulinzi wa amani.

"Sambamba na juhudi za mageuzi zinazoendelea, hasa katika mkakati wa amani na mabadiliko ya kidijitali, kutoka Accra, lazima tutengeneze uwezo mpya na wa ziada wenye utendaji wa hali ya juu na maalum, kuongeza ushirikiano endelevu, na kuweka dira kuelekea kuwa na chombo cha kulinda amani chenye nguvu na chenye uwajibikaji zaidi, " Bawumia amesema.

Pia amesisitiza dhamira isiyoyumba ya Ghana katika kuimarisha ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa na kutarajia mijadala zaidi kuhusu ajenda mpya ya amani, akitumai kuwa mkutano huo utatoa msukumo mpya wa ulinzi wa amani na ufanisi wa kutuma askari wa kulinda amani.

Kwenye mkutano huo wa siku moja, wajumbe walitarajiwa kujadili mada mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kulinda raia, mawasiliano ya kimkakati, usalama na ulinzi, afya ya akili ya walinda amani, na jukumu lisilo na mbadala la wanawake katika ulinzi wa amani.

Wajumbe wakiwa katika picha ya pamoja kwenye Mkutano wa Mawaziri wa Kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa wa Mwaka 2023 mjini Accra, Ghana, Desemba 6, 2023. (Picha na Seth/Xinhua)

Wajumbe wakiwa katika picha ya pamoja kwenye Mkutano wa Mawaziri wa Kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa wa Mwaka 2023 mjini Accra, Ghana, Desemba 6, 2023. (Picha na Seth/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha