

Lugha Nyingine
Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko na maporomoko ya udongo nchini Tanzania yafikia 69
(CRI Online) Desemba 07, 2023
Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko na maporomoko ya udongo kaskazini mwa Tanzania imeongezeka na kufikia 69 baada ya waokoaji siku ya Jumatano kuopoa miili minne kutoka kwenye tope lililosababishwa na maporomoko hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari katika mji wa Katesh, Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanazania na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Mobhare Matinyi amesema, wataalamu wa jiolojia wa Wizara ya Madini na Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) wamesema maafa hayo hayakusababishwa na milipuko ya volcano.
Kwa mujibu wa wataalamu hao, miamba kwenye milima ya Hanang ilizidiwa na maji mengi yaliyotokana na mvua kubwa iliyonyesha na kusababisha maporomoko hayo ya udongo na tope.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma