Waziri Mkuu wa China aongoza kwa pamoja na viongozi wa Umoja wa Ulaya Mkutano wa 24 wa Viongozi wa China na Umoja wa Ulaya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 08, 2023

Waziri Mkuu wa China Li Qiang (Katikati), Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel (Kushoto), na Rais wa Kamisheni ya Ulaya Ursula von der Leyen wakiwa katika picha wakati wa kuongoza kwa pamoja Mkutano wa 24 wa Viongozi wa China na Umoja wa Ulaya kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Desemba 7, 2023 (Xinhua/Liu Weibing)

Waziri Mkuu wa China Li Qiang (Katikati), Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel (Kushoto), na Rais wa Kamisheni ya Ulaya Ursula von der Leyen wakiwa katika picha wakati wa kuongoza kwa pamoja Mkutano wa 24 wa Viongozi wa China na Umoja wa Ulaya kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Desemba 7, 2023 (Xinhua/Liu Weibing)

Beijing - Waziri Mkuu wa China Li Qiang, Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel, na Rais wa Kamisheni ya Ulaya Ursula von der Leyen wameongoza kwa pamoja Mkutano wa 24 wa Viongozi wa China na Umoja wa Ulaya mjini Beijing siku ya Alhamisi ambapo Li amesema pande hizo mbili zinapaswa kuendelea kujikita katika kufanya mazungumzo badala ya mapambano, ushirikiano badala ya kutengana kiuchumi, na amani badala ya migogoro, ili kuongoza mwelekeo wa uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya.

Amesema China iko tayari kushirikiana na Umoja wa Ulaya ili kushikilia msimamo sahihi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote, kutafuta maelewano ya pamoja huku zikiondoa tofauti, kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana na utaratibu wa pande nyingi, kuufanya uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya kuwa thabiti, wa kiujenzi na wenye kunufaishana zaidi na kutoa mchango zaidi kwa ustawi, utulivu, na maendeleo ya Ulaya na Asia, Eurasia na Dunia kwa ujumla.

Li amesema kuwa China iko tayari kutafuta kikamilifu namna za ushirikiano wa kunufaishana na Umoja wa Ulaya na kujitahidi kuendelea kuingiza kasi na uhai mpya katika uhusiano wa pande mbili.

"Tutapanua zaidi biashara na uwekezaji kwa pande zote mbili, kuendelea kuongeza biashara na uwekezaji huria na urahisi, kuimarisha ushirikiano wa kijani, kuanzisha kikamilifu ushirikiano wa kidijitali, na kuimarisha mabadilishano kati ya watu," Li amesema huku akisema China inapinga ukiukwaji wa kanuni za msingi za uchumi wa soko na inapinga kuingiza siasa katika masuala ya uchumi na biashara au kuvumisha dhana ya usalama.

Pande hizo mbili zimekubaliana masuala mbalimbali ya kufanya kwa pamoja ikiwa ni pamoja na kupinga kutengana kiuchumi, kuweka mazingira ya biashara yaliyo ya haki na yasiyo ya kibaguzi kwa kampuni za kila pande, na kutatua ipasavyo tofauti kupitia mazungumzo na mashauriano. Pia zimekubaliana kuongeza ushirikiano katika uchumi na biashara, maendeleo ya kijani, kujenga ushirikiano thabiti wa mnyororo wa ugavi na utaratibu wa pande nyingi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha