China yafanya juhudi zote kuwezesha mafanikio ya mkutano "mgumu zaidi" wa Tabianchi wa Umoja wa Mataifa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 11, 2023

Mjumbe maalum wa China kuhusu mabadiliko ya Tabianchi Xie Zhenhua akizungumza kwenye  shughuli iliyofanyika  katika Banda la China la Mkutano wa Tabianchi wa COP28 mjini Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu, Desemba 8, 2023. (Xinhua/Wang Dongzhen)

Mjumbe maalum wa China kuhusu mabadiliko ya Tabianchi Xie Zhenhua akizungumza kwenye shughuli iliyofanyika katika Banda la China la Mkutano wa Tabianchi wa COP28 mjini Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu, Desemba 8, 2023. (Xinhua/Wang Dongzhen)

DUBAI - China inazungumza na pande zote husika ili kutafuta suluhu inayokubalika kwa wote na kuwezesha mafanikio ya Mkutano wa COP28, ambao unachukuliwa kuwa "mkutano mgumu zaidi" wa Tabianchi katika miaka ya hivi karibuni, mjumbe maalum huyo wa China kuhusu mabadiliko ya Tabianchi, Xie Zhenhua amesema huku akiongeza kuwa ameshiriki katika majadiliano ya Tabianchi kwa miaka 16, magumu zaidi ni ya mkutano wa mwaka huu.

Xie alikuwa akizungumzia Mkutano wa 28 wa Nchi Watia saini wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, ambao ulianza Novemba 30 na utafikia tamati Desemba 12.

Ameviambia vyombo vya habari kwamba mada zote ziliwasilishwa na kujadiliwa kikamilifu katika wiki ya kwanza ya mkutano huo, na kutolewa kwa toleo la kwanza la mswada wa nyaraka. Toleo hilo, lenye kurasa 27 kwa jumla, linajumuisha masuala zaidi ya 200 yanayohitaji kutatuliwa.

Xie amesema, kwa sasa, China iko katika mashauriano ya kina na pande zote kuu ili kupata makubaliano ambayo yanaendana na misingi ya Makubaliano ya Paris, yanayoakisi mwelekeo wa jumla wa mageuzi ya nishati, na yanaweza kuashiria mwelekeo sahihi wa juhudi za siku zijazo, na yatakuwa makubaliano yanayoonesha jumuishi zaidi.

"Tumepata maendeleo yenye hamasa. Tuna imani kubwa juu ya hili," Xie amesisitiza.

Watembeleaji wakipiga picha mbele ya Banda la China kwenye Eneo la Kijani la Mkutano wa 28 wa Nchi Watia saini wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28), mjini Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu, Desemba 3, 2023 (Xinhua/Wang Dongzhen)

Watembeleaji wakipiga picha mbele ya Banda la China kwenye Eneo la Kijani la Mkutano wa 28 wa Nchi Watia saini wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28), mjini Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu, Desemba 3, 2023 (Xinhua/Wang Dongzhen)

Hata hivyo, ameongeza, kubadilisha muundo wa nishati kunaweza kuwa mchakato wenye uchungu, kwani kila nchi ina hali yake maalum, ina muundo wake wa nishati na majaliwa ya rasilimali, na watu wanatakiwa kukumbuka barabara usalama wa nishati, chakula na uchumi, hili ni sharti la kwanza la kubadilisha muundo wa nishati katika hali tulivu.

Xie amesisitiza kwamba katika mchakato wa kubadilisha muundo wa nishati, nchi zote "zinapaswa kuelewana na kuungana mkono, kujifunza kutoka kwa nguvu za kila mmoja, kutafuta suluhisho bora la matatizo kwa kuimarisha ushirikiano wa kimataifa."

Kuhusu hatua za China katika kutekeleza malengo ya Makubaliano ya Paris, Xie amesema China itafikia kilele cha utoaji wa kaboni kabla ya Mwaka 2030 na imetoa mchango mkubwa kwa Dunia katika kubadilisha muundo wa nishati na kwa ajili ya maendeleo ya nishati mbadala.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha