

Lugha Nyingine
“Mzunguko wa Buluu”, hatua mpya ya China ya kuondoa takataka za plastiki baharini
Wahudumu wakikusanya takataka za plastiki kwenye Kisiwa cha Dachen cha Mji wa Taizhou katika Mkoa wa Zhejiang, China. (Picha kwa hisani ya mradi wa “Mzunguko wa Buluu”)
Katika uteuzi uliotangazwa hivi karibuni wa “Tuzo ya Walinzi wa Dunia” ya Umoja wa Mataifa 2023, mfumo wa "Mzunguko wa Buluu" ambao umeanzishwa katika Mkoa wa Zhejiang wa China umejitokeza kati ya miradi 2,500 duniani, na kushinda heshima ya juu zaidi ya Umoja wa Mataifa katika nyanja ya kulinda mazingira ya asili. Katika utekelezaji wa mradi huo, takataka za plastiki zenye uzito wa tani 2,254 hivi zimekusanywa na kushughulikiwa, kazi hii imepunguza utoaji wa kaboni kwa tani 2,930 hivi, na kuboresha kwa ufanisi mazingira ya pwani.
Mfumo huo umekuwa ukitekelezwa mkoani Zhejiang kuanzia Mwaka 2020. Kupitia “uelekezaji wa serikali + uendeshaji wa soko” umevutia wakazi wa pwani kushiriki katika kukusanya takataka za plastiki kutoka baharini, kushirikiana na kampuni za kutengeneza bidhaa za plastiki, kuanzisha “Mfuko wa Kustawi Pamoja wa Umoja wa Buluu” kwa ajili ya kugawana thamani ya pili ya kazi, na kutimiza malengo mawili ya kulinda mazingira ya asili na kuongeza kipato cha wakazi.
Mvuvi akikusanya takataka za baharini ili kuziweka wenye ngalawa ya kukusanya takataka katika Gati la Yuncang lililoko Mji wa Zhoushan, Mkoa wa Zhejiang. (Chanzo cha picha: UNEP)
Katika Mji wa Wenling mkoani Zhejiang, Li Qiming mwenye umri wa miaka 54 kila baada ya kufanya kazi yake katika kiwanda cha kutengeneza mazao ya majini, hukusanya chupa za plastiki sehemu za pwani na kuziuza ili kuikimu familia yake. Mfumo wa “Mzunguko wa Buluu” umepandisha bei ya uuzaji wa takataka za plastiki baharini. Wavuvi wenyeji siyo tu huwasilisha samaki sokoni, bali pia mara kwa mara huleta takataka za plastiki kwenye “nyumba ndogo za buluu”, ambazo ni vituo vya kuwekwa kwa takataka za plastiki zilizokusanywa kutoka baharini.
Kwa sasa “nyumba ndogo za buluu” 15 zimeanzishwa katika miji ya Taizhou, Ningbo na Zhoushan ya Mkoa wa Zhejiang. Vituo hivi vinashughulikia takataka hizi kwa hatua ya kwanza, hivyo vimepunguza kwa kiasi kikubwa gharama za usafirishaji na kazi ya kushughulikiwa.
Wafanyakazi wakishughulikia chupa za plastiki zilizokusanywa kwenye “Nyumba Ndogo ya Buluu” katika eneo la Jiaojiang la Mji wa Taizhou, Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China, Oktoba 17, 2023. (Xinhua/Lin Guangyao)
Katika kiwanda cha kisasa cha kutumia plastiki tena cha Kampuni ya Teknolojia ya Veolia Huafei ya Zhejiang, takataka za plastiki kutoka baharini hupitia michakato ya kutengenezwa kwa hatua tatu, na kubadilika kuwa chembe za plastiki zinazoweza kutumiwa tena, ambazo zinatumiwa katika kutengeneza raslimali za nguo, bihaa za ufungaji, vipuri vya magari na bidhaa nyingine.
Chembe za plastiki zinazoweza kutumika tena. (Chanzo cha picha: UNEP)
Kwa sasa viwanda na kampuni 237 na meli 10,200 zimejiunga na “Mzunguko wa Buluu”. Wanawake, wazee na wavuvi wanaoishi sehemu za pwani wameshiriki kwa hamasa kwenye mradi huo, na idadi ya washiriki imezidi 60,000. Katika utekelezaji wa mradi wa “Mzunguko wa Buluu”, kwa jumla kumekusanywa na kushughulikiwa takataka baharini za aina mbalimbali kwa tani zaidi ya 10,000.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma