Rais Xi asema China na Vietnam ziko kwenye njia yenye matumaini ya kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 12, 2023

Beijing - Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Chama cha Kikomunisti cha Vietnam (CPV) na nchi hizo mbili zimepata njia yenye matumaini ya kujenga kwa pamoja jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja, Rais wa China Xi Jinping amesema katika makala iliyotiwa saini yake ambayo imechapishwa kwenye Gazeti la Nhan Dan la Vietnam siku ya Jumanne kabla ya ziara yake nchini humo.

Mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 15 tangu kuanzishwa kwa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Vietnam, Rais Xi amesema katika makala hiyo yenye kichwa "Kujenga Jumuiya Yenye Umuhimu wa Kimkakati ya China na Vietnam ya Mustakabali wa Pamoja, Kufungua Ukurasa Mpya wa Kushirikiana Kuelekea Maendeleo ya Mambo ya Kisasa."

Katika makala yake hiyo Rais Xi amesema, "Haijalishi mazingira ya kimataifa yanavyobadilika kwa namna gani, vyama vyetu na nchi zetu mbili zimeshirikiana kudumisha amani na utulivu, kutafuta maendeleo na ushirikiano, na kuleta ustawi na maendeleo. Tumepata njia yenye matumaini ya kujenga kwa pamoja jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja".

Amesema, nchi hizo mbili zimeimarisha maslahi yao ya pamoja kwa ushirikiano wa kunufaishana. Kwa muda mrefu China imekuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Vietnam, na Vietnam ni mshirika mkubwa wa kibiashara wa China katika Umoja wa nchi za Asia ya kusini mashariki na ya nne kwa ukubwa duniani.

Nchi hizo mbili zimekuwa na uhusiano wa karibu kwa kupitia mawasiliano ya kirafiki kati ya watu wao. Usafiri wa watu wa nchi hizo mbili umerejea haraka kwa uimara mwaka huu. Kuanzia Januari hadi Oktoba, watalii wa China wamefanya safari za kitalii zaidi ya milioni 1.3 nchini Vietnam, amesema.

Amesema, siku zote nchi hizo mbili zimetendeana kwa udhati na kama watetezi wawili wa ushirikiano wa pande nyingi, China na Vietnam zinathamini umuhimu wa mazungumzo, mashauriano na ushirikiano wa amani, na kushikilia kithabiti kanuni za kimsingi za uhusiano wa kimataifa zilizowekwa kwenye msingi wa nia na kanuni za “Katiba ya Umoja wa Mataifa".

"Tunasaidiana katika masuala yanayohusu masilahi yetu ya kimsingi na mambo tunayojali zaidi, na kudumisha uratibu wa karibu katika mifumo ya ushirikiano wa kikanda na kimataifa," amesema.

Rais Xi amesema, Vietnam ni mshiriki muhimu katika Kikundi cha Marafiki wa Pendekezo la Maendeleo ya Dunia (GDI). Inaunga mkono Pendekezo la Usalama wa Dunia (GSI) na Pendekezo la Ustaarabu wa Dunia (GCI), na inaunga mkono China kujiunga na Mkataba wa Uhusiano wa Wenzi wa Pande zote na Maendeleo wa Kuvuka Eneo la Pasifiki".

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha