Idadi ya Maeneo ya Kitaifa ya Maendeleo ya Viwanda vya Teknolojia ya Hali ya juu nchini China yaongezeka hadi 178

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 13, 2023

Picha hii ya angani iliyopigwa Septemba 10, 2023 ikionyesha mandhari ya eneo la Zhangjiang katika Eneo la Majaribio ya Biashara Huria la China (Shanghai) mjini Shanghai, Mashariki mwa ya China. (Xinhua/Fang Zhe)

Picha hii ya angani iliyopigwa Septemba 10, 2023 ikionyesha mandhari ya eneo la Zhangjiang katika Eneo la Majaribio ya Biashara Huria la China (Shanghai) mjini Shanghai, Mashariki mwa ya China. (Xinhua/Fang Zhe)

Beijing – Idadi ya jumla ya Maeneo ya Kitaifa ya Maendeleo ya Viwanda vya Teknolojia ya Hali ya juu nchini China imefika 178 hadi kufikia mwishoni mwa Novemba, Wu Jiaxi, Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Mipango katika Wizara ya Viwanda na TEHAMA ya China amesema Jumanne huku akiongeza kuwa katika robo tatu za kwanza za mwaka huu, pato la kiuchumi la maeneo hayo lilifikia yuan trilioni 12.33 (sawa na dola za kimarekani trilioni 1.73), ikiwa ni ongezeko la asilimia 7.11 kwa mwaka.

"Kutegemea maeneo ya kitaifa ya teknolojia ya hali ya juu, vikundi kadhaa vya viwanda vya teknolojia ya hali ya juu vimeanzishwa na kuendelezwa, na kuwa nguvu muhimu katika kuhimiza maendeleo ya viwanda vipya na kuhakikisha usalama wa minyororo ya uzalishaji na ugavi," Wu amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Beijing.

Takwimu zilizotolewa kwenye mkutano huo zinaonyesha kuwa katika miaka ya hivi karibuni, maeneo hayo yamekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo yenye ubora wa juu na kuwa injini muhimu ya maendeleo ya kiuchumi.

Takwimu zinaonesha kuwa, wakati huo huo, maeneo haya yamekusanya asilimia karibu 80 ya maabara muhimu za kitaifa na asilimia 70 ya vituo vya kitaifa vya uvumbuzi wa viwanda. Wakati huo huo, idadi kubwa ya mafanikio asili yanayoongozwa, kama vile roboti za akili bandia na urambazaji wa satelaiti, yanaharakisha maendeleo ya viwanda katika maeneo ya teknolojia ya hali ya juu.

Wu amesema kuwa wizara yake itahimiza maeneo hayo yenye sifa zinazostahili kujenga vituo kadhaa vya uingizaji kwenye viwanda mafanikio ya sayansi na teknolojia, ili kuhamisha mafanikio zaidi ya sayansi kutoka maabara hadi kwenye mistari ya uzalishaji viwandani.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha