Mradi mkubwa wa reli wa Malaysia waanza kutandaza njia ya kwanza ya reli

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 13, 2023

Mfalme wa Malaysia Sultan Abdullah Sultan Ahmad Shah akishuhudia uwekaji wa njia ya Reli  kwenye Pwani ya Mashariki (East Coast Rail Link)  huko Kuantan, Malaysia, Desemba 11, 2023. (Picha na Chong Voon Chung/Xinhua)

KUANTAN - Mradi wa Reli kwenye Pwani ya Mashariki (ECRL) ambao ni mradi mkubwa wa reli nchini Malaysia unaojengwa na Kampuni ya Ujenzi wa Mawasiliano ya China (CCCC) umetandaza njia ya kwanza ya reli siku ya Jumatatu wiki hii ambapo Mfalme wa Malaysia Sultan Abdullah Sultan Ahmad Shah ni miongoni mwa wageni walioshuhudia tukio hilo la kihistoria na kukata utepe rasmi kuashiria kuanza kwa kazi ya utandazaji wa njia hiyo ya reli.

Waziri wa Uchukuzi wa Malaysia Loke Siew Fook akizungumza kwenye hafla ya ukataji utepe kuashiria kuanza kwa kazi ya uwekaji wa njia ya Reli  kwenye Pwani ya Mashariki (East Coast Rail Link)  huko Kuantan, Malaysia, Desemba 11, 2023. (Picha na Chong Voon Chung/Xinhua)

Katika hotuba yake kwenye hafla hiyo, Waziri wa Uchukuzi wa Malaysia Loke Siew Fook amepongeza mradi huo kwa manufaa yake ya kiuchumi kwa Malaysia, na kuhimiza maendeleo ya maeneo ya pwani ya mashariki ya nchi hiyo, na pia amesifu mradi huo kuleta uwezekano wa kuongeza ustadi wa ufundi na kuhamisha teknolojia.

Pia amesema vifaa vya hali ya juu vya kuweka njia za reli kutoka China vinasaidia sana katika kuboresha ufanisi wa ujenzi wa reli hiyo. "Mashine ya kutandaza njia za reli inakadiriwa kutandaza takriban njia za reli zenye urefu wa kilomita 1.5 kwa siku."

Picha hii iliyopigwa Desemba 11, 2023 ikionyesha hafla ya ukataji utepe kuashiria kuanza kwa uwekaji wa njia ya Reli  kwenye Pwani ya Mashariki (East Coast Rail Link) mjini Kuantan, Malaysia, Desemba 11, 2023. (Picha na Chong Voon Chung/Xinhua)

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCCC Wang Tongzhou amesema utandazaji wa njia ya reli unaashiria kupiga hatua kwa mradi kutoka kwenye ujenzi wa chini ya ardhi hadi ujenzi wa juu ya ardhi.

Amesema CCCC itaendelea kuwekeza rasilimali bora ili kuharakisha ujenzi wa mradi huo na kuimarisha zaidi ushirikiano wa pande zote na Malaysia, ikiendana na mipango ya maendeleo ya serikali ya Malaysia.

"Lengo letu ni kufanya mradi wa ECRL kuwa alama ya ushirikiano wa kudumu na wa kirafiki kati ya nchi zetu mbili," amesema.

Ukiwa ni mradi mkubwa wa miundombinu chini ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI), ECRL inaanzia katika kituo kikuu cha usafiri cha Malaysia cha Port Klang na kutandazwa kupitia peninsula nzima hadi Jimbo la Kelantan, Kaskazini Mashariki mwa Malaysia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha