Rais Xi asema ziara yake ya kiserikali nchini Vietnam imefikia kilele cha mafanikio ya juhudi za kidiplomasia za China Mwaka 2023

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 14, 2023

Rais wa China Xi Jinping ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mkewe, Peng Liyuan wakiagana na Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam Nguyen Phu Trong na mkewe, Ngo Thi Man, kabla ya kurudi China baada ya kufanya ziara ya kiserikali nchini Vietnam, Desemba 13, 2023. (Xinhua/Shen Hong)

Rais wa China Xi Jinping ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mkewe, Peng Liyuan wakiagana na Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam Nguyen Phu Trong na mkewe, Ngo Thi Man, kabla ya kurudi China baada ya kufanya ziara ya kiserikali nchini Vietnam, Desemba 13, 2023. (Xinhua/Shen Hong)

HANOI - Katika hotuba yake wakati yeye na mkewe Peng Liyuan, wakiagana na Nguyen Phu Trong, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam na mkewe, Ngo Thi Man, kabla ya kurudi China, Rais wa China Xi Jinping amesema, muda mfupi baada ya Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kuhitimishwa kwa mafanikio mwishoni mwa Oktoba, 2022, Nguyen Phu Trong alikuwa kiongozi wa kwanza wa kigeni kuitembelea China na kwamba wakati huu, ziara yake ya kiserikali nchini Vietnam imefikia kilele cha mafanikio ya juhudi za kidiplomasia za China Mwaka 2023, ambayo ni yenye umuhimu wa kimkakati.

Rais Xi ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC amesema katika miaka mingi iliyopita, viongozi wa vyama na nchi hizo mbili wamedumisha mawasiliano ya karibu kila wakati, wakifikia makubaliano mengi muhimu ya kuongoza maendeleo ya ushirikiano na uhusiano kati ya China na Vietnam.

Huku akieleza kuwa ni utamaduni mzuri kwa viongozi wa vyama hivyo viwili kuandaa mipango ya maendeleo ya uhusiano kati ya vyama na nchi hizo mbili, Rais Xi ameeleza kuwa katika ziara yake hiyo yeye na Trong kwa pamoja wametangaza ujenzi wa jumuiya ya China na Vietnam yenye mustakabali wa pamoja, ambayo ina umuhimu wa kimkakati.

Katika ziara hiyo ya Rais Xi, viongozi hao wawili walinukuu mara kadhaa kauli maarufu ya kiongozi wa zamani wa Vietnam marehemu Ho Chi Minh, ambayo iliuelezea uhusiano wa China na Vietnam kama mshikamano wa "urafiki na undugu."

Rais Xi amesema kilichomvutia zaidi ni msisitizo wa mara kwa mara wa Trong kwamba uhusiano wa "urafiki na undugu" kati ya China na Vietnam ni mwanzo na msingi wa uhusiano wa China na Vietnam.

Maadamu pande hizo mbili zinaendelea kufuata njia hii kwa uthabiti, uhusiano kati ya China na Vietnam hakika utafikia maendeleo mapya, na kuleta manufaa zaidi kwa watu wa nchi zote mbili, Rais Xi amesema, huku akimshukuru Nguyen Phu Trong na mkewe kwa "mapokezi mazuri na yenye ukarimu mkubwa zaidi" katika ziara hiyo.

Alipokuwa akiwaaga Xi na mkewe, Trong amempongeza Rais Xi kwa mafanikio makubwa ya ziara yake hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha