Zaidi ya nusu ya miradi ya ushirikiano iliyofikiwa kwenye Mkutano wa BRF yaanza kutekelezwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 15, 2023

Picha hii iliyopigwa Oktoba 14, 2023 ikionyesha mapambo ya maua kwa ajili ya Mkutano wa 3 wa Baraza la Ushirkiano wa Kimataifa wa Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRF) karibu na Kituo cha Mikutano cha Taifa cha China mjini Beijing, China. (Xinhua/Ju Huanzong)

Picha hii iliyopigwa Oktoba 14, 2023 ikionyesha mapambo ya maua kwa ajili ya Mkutano wa 3 wa Baraza la Ushirkiano wa Kimataifa wa Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRF) karibu na Kituo cha Mikutano cha Taifa cha China mjini Beijing, China. (Xinhua/Ju Huanzong)

BEIJING - Zaidi ya nusu ya jumla ya miradi 369 ya ushirikiano iliyofikiwa kwenye Mkutano wa 3 wa Baraza la Ushirikiano wa Kimataifa wa Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRF) imeanza kutekelezwa kwa sasa, kwa mujibu wa taarifa ya Kamati ya Taifa ya Maendeleo na Mageuzi ya China (NDRC) iliyotolewa siku ya Alhamisi.

Idara inayohusika na ujenzi wa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja chini ya NDRC inasema, utekelezaji huo wa miradi ya ushirikiano umeimarisha kuaminiana kisiasa, ushirikiano wa kiuchumi na mabadilishano ya watu kati ya China na nchi husika na mashirika ya kimataifa.

China imetia saini nyaraka za ushirikiano na nchi mbalimbali zikiwemo Honduras, Argentina, Mauritania, Serbia, na Misri, na kuimarisha na kupanua zaidi ushirikiano katika ujenzi wa Ukanda Mmoja, Njia Moja.

China pia imetia saini nyaraka za ushirikiano na mashirika ya kimataifa, yakiwemo ya Umoja wa Mataifa, Shirika la Haki Miliki Duniani, na Shirika la Hali ya Hewa Duniani, ili kuimarisha ushirikiano katika masuala ya uchukuzi endelevu, haki miliki na hali ya hewa.

Wakati huo huo, miradi ya ushirikiano, kama vile ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Siem Reap Angkor nchini Cambodia na uwekezaji wa Eneo la Ushirikiano wa Kiuchumi la Jiangxi nchini Zambia, umeongeza maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi hizi, kwa mujibu wa NDRC.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha