China yaipatia Uganda magari ya SUV ili kuiunga mkono kuandaa mkutano wa NAM na wa Kusini

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 15, 2023

Maafisa wa Uganda na Balozi wa China nchini Uganda Zhang Lizhong wakishiriki kwenye hafla ya makabidhiano ya magari ya SUV mjini Kampala, Uganda tarehe 14, Desemba, 2023. (Picha kwa hisani ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Uganda na ilichapishwa na Xinhua)

Maafisa wa Uganda na Balozi wa China nchini Uganda Zhang Lizhong wakishiriki kwenye hafla ya makabidhiano ya magari ya SUV mjini Kampala, Uganda tarehe 14, Desemba, 2023. (Picha kwa hisani ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Uganda na ilichapishwa na Xinhua)

China imeahidi kuiunga mkono Uganda wakati nchi hiyo inapofanya maandalizi kwa ajili ya kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 19 wa Nchi Wanachama wa Harakati ya Kutofungamana na Upande wowote (NAM) na Mkutano wa tatu wa Kusini. Ahadi hiyo imetangazwa na Balozi wa China nchini Uganda Zhang Lizhong Alhamisi alipokuwa akikabidhi magari 70 ya SUV kwa serikali ya Uganda.

Zhang amesema China itaendelea kuiunga mkono Uganda kutoa mchango muhimu zaidi katika mambo ya kikanda na ya kimataifa, na kuimarisha mshikamano kati ya nchi zinazoendelea kupitia mikutano hiyo.

“Makabidhiano haya ya magari 70 ni mfano mwingine mpya wa uungaji mkono wa China kwa Uganda bila kuyumbayumba,” amesema balozi huyo.

Kabla ya hapo China ilikuwa imetoa magari 70 ya SUV kwa ajili ya mikutano hiyo ijayo iliyopangwa kufanyika mwezi wa Januari, 2024.

Vincent Bagiire, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uganda amesema nchi hiyo inatarajia ujumbe wa watu kutoka nchi 120 kwa ajili ya mkutano wa NAM na kutoka nchi 134 kwa ajili ya mkutano wa Kusini.

“Tunapenda kuishukuru China kwa kutupatia magari haya. China na Uganda zimeshirikiana katika miradi mbalimbali ya miundombinu. Upanuzi wa uwanja wetu wa ndege (Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe) unaotekelezwa na kampuni ya China utakamilika mwezi huu,” amesema Bagiire.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha