Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya apongeza miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia wa Kenya na China

(CRI Online) Desemba 15, 2023

Mkuu wa Mawaziri ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Bw. Musalia Mudavadi akiwa katika mahojiano ya pamoja na vyombo vya habari vya China mjini Nairobi, Kenya Tarehe 11, Desemba. (Picha na Li Yahui/Xinhua)

Kenya na China zimeadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia siku ya Alhamisi Desemba 14.

Mkuu wa Mawaziri ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje ya Kenya, Bw. Musalia Mudavadi amesema, katika miaka 60 iliyopita, uhusiano kati ya Kenya na China umepata maendeleo makubwa, kuaminiana kisiasa kumeongezeka, na uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya pande hizo mbili umeendelea kuimarika.

Amesema ujenzi wa pamoja wa Pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na mipango mingine inaunganisha kwa kina mawazo ya China na Dira ya Maendeleo ya Kenya ya mwaka 2030.

Bw. Mudavadi pia amesema Kenya inatarajia kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, kuimarisha mabadilishano kati ya watu, na kuungana mkono ili kuingia katika miaka mingine 60 mipya.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha