UNESCO na Huawei zashirikiana pamoja na kukabidhi vifaa vya ICT katika shule za nchini Ethiopia

(CRI Online) Desemba 15, 2023

Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) na kampuni kubwa ya mawasiliano ya China, Huawei, zimeshirikiana na kutoa vifaa vya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kwa Wizara ya Elimu ya Ethiopia.

Katika taarifa iliyotolewa jana, kampuni ya Huawei imesema hatua hiyo ni sehemu ya uratibu wa pamoja wa UNESCO na Huawei chini ya mradi wa Mfumo Wazi wa Shule kwa Wote unaowezeshwa na Teknolojia (TeOSS).

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa hivyo, Waziri wa Elimu wa nchini Ethiopia, Ayelech Eshete ameipongeza UNESCO na Huawei kwa ahadi yao kuhusu suala la elimu na kwa kushirikisha wazo lao la jamii jumuishi ya kidijitali.

Mwakilishi wa UNESCO nchini Ethiopia, Rita Bissoonauth amesema, Shirika hilo pamoja na kampuni ya Huawei na Wizara ya Elimu ya Ethiopia, zimeanzisha mradi huo ili kupunguza pengo la kidijitali na kuanzisha mfumo wa shule unaoweza kukabiliana na migogoro.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha