Maoni ya Katuni kuhusu Sheria ya Kupunguza Mfumuko wa Bei ya Marekani: "Inakosesha"

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 15, 2023

Mchoraji wa katuni: Ma Hongliang (Katuni hii ni hakimiliki ya People's Daily Online, tafadhali usiichapishe bila idhini.)

Mchoraji wa katuni: Ma Hongliang (Katuni hii ni hakimiliki ya People's Daily Online, tafadhali usiichapishe bila idhini.)

Hivi karibuni, serikali ya Marekani ilitoa maelezo kuhusu utekelezaji wa sera ya ruzuku ya magari yanayotumia nishati ya umeme chini ya "Sheria ya Kupunguza Mfumuko wa Bei."

Kwa mujibu wa maelezo yake, magari ya umeme ya Marekani yanayoundwa na vipengele vya betri vilivyotengenezwa au kuunganishwa sehemu zake katika nchi kama vile China hayatasamehewa ushuru.

Kitendo hiki ni Marekani kuingiza siasa katika masuala husika ya kiuchumi, kuweka vikwazo vya kibiashara katika mnyororo wa ugavi wa betri, na kukandamiza mnyororo wa viwanda vya nishati mpya vya China. Chombo cha habari cha Bloomberg kiliripoti hapo awali kwamba takwimu zinaonyesha kuwa kampuni za China zinachukua zaidi ya nusu ya soko la kimataifa la betri za magari ya umeme, na utoaji wake wa baadhi yamalighafi za kutengeneza betri umekidhi 90% ya mahitaji.

kitendo hiki cha Marekani imevuruga kwa kiasi kikubwa minyororo ya kimataifa ya uzalishaji na ugavi na kuzidisha hatari ya kugawanyika kwa uchumi wa Dunia. Ushindani unapaswa kuwa wa haki na wenye maana, na Marekani inapaswa kutimiza kikamilifu wajibu wake chini ya sheria za Shirika la Biashara Duniani (WTO) na kulinda kikamilifu mamlaka na ufanisi wa mfumo wa biashara wa pande nyingi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha