Rais Xi Jinping atuma salamu za rambirambi kwa Amiri mpya Sheikh Mishal kufuatia kifo cha Amiri wa Kuwait Sheikh Nawaf

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 18, 2023

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ametuma salamu za rambirambi Jumapili kwa Amiri mpya wa Kuwait Sheikh Mishal Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah kufuatia kifo cha Amir Sheikh Nawaf Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah akisema kuwa kwa niaba ya Serikali na watu wa China na vile vile kwa jina lake mwenyewe, anatoa salamu za rambirambi kwa kuondokewa na Sheikh Nawaf na anatoa salamu za dhati za pole kwa familia yake na watu wa Kuwait.

Katika ujumbe wake, Rais Xi amesema Sheikh Nawaf anaheshimiwa na kupendwa na watu wa Kuwait na ametoa mchango kwa ajili ya kuendeleza uhusiano kati ya China na Kuwait.

Huku akieleza kuwa kuondokewa na Sheikh Nawaf ni hasara kubwa kwa watu wa Kuwait, Rais Xi amesema watu wa China pia wamempoteza rafiki mpendwa.

Rais Xi amesema, Serikali ya China na watu wa China wanathamini urafiki kati ya nchi hizo mbili, na kuamini kwamba kwa juhudi za pamoja za pande zote mbili, uhusiano wa kimkakati wa China na Kuwait utaimarishwa na kuenelezwa kwa hatua madhubuti.

Katika siku hiyo ya Jumapili Waziri Mkuu wa China Li Qiang pia alituma salamu za rambirambi kwa Waziri Mkuu wa Kuwait Sheikh Ahmad Nawaf Al-Ahmad Al-Sabah kufuatia kifo cha Sheikh Nawaf, na kutoa salamu za rambirambi kwa serikali ya Kuwait na salamu za dhati za pole kwa familia ya marehemu Amiri.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha