

Lugha Nyingine
China yasisitiza ukaguzi wa njia za treni za sabwei, vifaa vingine kutokana na kuwepo kwa baridi kali
Magari ya kuondoa theluji yakiondoa theluji barabarani mjini Yantai, katika Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China, Desemba 16, 2023. (Picha na Tang Ke/Xinhua)
Beijing – Kamati ya kitaifa ya China ya kuzuia, kupunguza na kutoa msaada wakati wa majanga siku ya Jumapili imetoa wito wa kuimarishwa ukaguzi wa njia za treni za sabwei, barabara za juu, njia za handaki za waenda kwa miguu na barabara ambazo zinaathirika kirahisi kwa barafu ili kuzuia ipasavyo ajali kutokana na kuwepo kwa baridi kali.
Juhudi zaidi zinapaswa kufanywa ili kuimarisha ufuatiliaji, utabiri wa hali ya hewa na utoaji wa tahadhari, na kuanzisha mwitikio wa dharura kwa wakati muafaka, kamati hiyo imesema katika waraka wake kwa serikali za mitaa.
Waraka huo umesema ni muhimu kuimarisha ufuatiliaji wa uendeshaji wa gridi ya umeme, ili kuhakikisha usalama wa nishati kwa kuongeza uzalishaji na utoaji wa bidhaa, na kutilia maanani kwa makini zaidi utoaji wa bidhaa na bei za bidhaa hizo ambazo ni muhimu kwa maisha ya watu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma