

Lugha Nyingine
Mwanadiplomasia Mwandamizi wa China Wang Yi akutana na wajumbe wa kidiplomasia kutoka nchi za ASEAN
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) akikutana na wajumbe wa kidiplomasia wa nchi za Umoja wa Nchi za Asia Kusini Mashariki (ASEAN) mjini Beijing, China, Desemba 15, 2023. Balozi wa Timor-Leste nchini China alihudhuria mkutano huo. (Xinhua/Liu Bin)
BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amekutana na wajumbe wa kidiplomasia kutoka Jumuiya ya Nchi za Asia Kusini Mashariki (ASEAN) mjini Beijing siku ya Ijumaa iliyopita, akitoa wito wa kuwepo kwa jumuiya ya karibu ya China na ASEAN yenye mustakabali wa pamoja.
Wang, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesema katika miaka 10 iliyopita, jumuiya ya China na ASEAN yenye mustakabali wa pamoja imekuwa karibu siku hadi siku. Amesema, pande hizo mbili zimepata mafanikio makubwa katika ujenzi wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, na kutekeleza kikamilifu dhana ya urafiki, udhati, manufaa ya pande zote na jumuishi katika uhusiano wa pande mbili.
Amesema, kama jirani mkubwa wa nchi za ASEAN, China itaendelea kuwa mshirika wa kimkakati wa kutegemewa na wa muda mrefu wa ASEAN ili kuendeleza kwa pamoja maendeleo ya kisasa ya Asia.
“China inaunga mkono ASEAN katika kutekeleza jukumu lake linalostahili kuhusu suala la Myanmar na iko tayari kushirikiana na nchi za ASEAN ili kuendeleza suluhu sahihi ya suala la Myanmar,” amesema.
Kwa upande wao, wajumbe hao wa kidiplomasia wa nchi za ASEAN wamesema, China imetoa fursa kubwa kwa nchi za ASEAN kupata amani, maendeleo na ustawi. Wamesema, nchi za ASEAN zinathamini uungaji mkono wenye thamani wa China, na zingependa kushirikiana na China ili kuhimiza kwa pamoja ujenzi wa Ukanda Mmoja, Njia Moja.
Nchi za ASEAN zingependa kupeleka uhusiano wa kimkakati wa pande zote wa ASEAN na China kwenye ngazi mpya, kujenga mustakabali mwema na endelevu zaidi wa uhusiano wa ASEAN na China, na kuchangia katika amani na maendeleo ya kikanda, wajumbe hao wameongeza.
Balozi wa Timor-Leste nchini China alihudhuria mkutano huo.
Wang pia alikutana na Balozi wa Cambodia anayemaliza muda wake nchini China Khek Caimealy Sysoda kwa wakati tofauti mjini Beijing siku hiyo ya Ijumaa.
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) akikutana na Balozi wa Cambodia anayemaliza muda wake nchini China Khek Caimealy Sysoda mjini Beijing, China, Desemba 15, 2023. (Xinhua/Liu Bin)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma