Uganda yafungua tena daraja muhimu la Katonga lililokarabatiwa na mkandarasi wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 18, 2023

Wafanyakazi wakikagua sehemu ya uharibifu uliotokana na mafuriko katika barabara kuu ya Kampala-Masaka, nchini Uganda, Mei 12, 2023. (Picha na Nicholas Kajoba/Xinhua)

Wafanyakazi wakikagua sehemu ya uharibifu uliotokana na mafuriko katika barabara kuu ya Kampala-Masaka, nchini Uganda, Mei 12, 2023. (Picha na Nicholas Kajoba/Xinhua)

KAMPALA - Uganda imefungua tena daraja muhimu la Katonga kwenye barabara kuu ya kimataifa inayounganisha nchi hiyo na nchi nyingine nne ambalo liliharibiwa na mafuriko mwezi Mei, na kukarabatiwa na kuboreshwa na Kampuni ya Ujenzi wa Mawasiliano ya China (CCCC).

Daraja hilo liko kwenye barabara kuu inayounganisha Uganda na nchi jirani za Tanzania, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Allan Ssempebwa, afisa mawasiliano katika Mamlaka ya Taifa ya Barabara ya Uganda, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kwa njia ya simu Jumamosi kwamba daraja hilo limefunguliwa tena Ijumaa.

"Wakati daraja liliposombwa na maji, tulifikiria kampuni ya haraka na yenye ufanisi ya kulikarabati. CCCC ilitujia akilini kwa sababu walifanya kazi kama hiyo nchini Uganda," Ssempebwa amesema. "Kwa teknolojia ya kisasa, wameweza kujenga daraja la chuma kwa muda mfupi iwezekanavyo ili kuweza kupitisha aina zote za magari."

"Barabara hii ni muhimu sana kwa sababu inaunganisha Uganda na nchi nyingine za kikanda," amesema. 

Picha hii iliyopigwa Mei 12, 2023, ikionyesha sehemu ya uharibifu uliotokana na mafuriko kwenye barabara kuu ya Kampala-Masaka, nchini Uganda. (Picha na Nicholas Kajoba/Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Mei 12, 2023, ikionyesha sehemu ya uharibifu uliotokana na mafuriko kwenye barabara kuu ya Kampala-Masaka, nchini Uganda. (Picha na Nicholas Kajoba/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha