Rajoelina aahidi kujenga Madagascar yenye nguvu na ustawi zaidi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 18, 2023

Andry Rajoelina (Kati), aliyechaguliwa tena kuwa Rais wa Madagascar, akihudhuria hafla ya kuapishwa kwake mjini Antananarivo, Madagascar, Desemba 16, 2023. (Picha na Sitraka Rajaonarison/Xinhua)

Andry Rajoelina (Kati), aliyechaguliwa tena kuwa Rais wa Madagascar, akihudhuria hafla ya kuapishwa kwake mjini Antananarivo, Madagascar, Desemba 16, 2023. (Picha na Sitraka Rajaonarison/Xinhua)

ANTANANARIVO - Rais aliyechaguliwa tena Andry Rajoelina wa Madagascar ameahidi kuiongoza nchi hiyo ili "kujenga taifa lenye nguvu na ustawi zaidi" katika hotuba yake kwa taifa kwenye hafla ya kuapishwa kwake iliyofanyika Jumamosi katika Uwanja wa Barea, mjini Antananarivo.

"Ninaahidi kuiongoza Madagascar kwa dhamira ili kujenga taifa lenye nguvu na ustawi zaidi, na kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo yake," Rajoelina amesema.

Akiwa alitangazwa Desemba 1 na Mahakama Kuu ya Kikatiba ya nchi hiyo kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais wa Novemba 16 kwa kupata asilimia 58.96 ya kura zote halali, Rajoelina amepongeza "ukomavu wa kidemokrasia" wa taifa hilo akibainisha kuwa mchakato huo umefanywa kwa utulivu, ikiwa ni "ishara ya taifa ambalo limedhamiria kuendelea katika mazingira ya amani na utulivu."

Kwenye hotuba yake, Rajoelina ametaja nguzo tatu – rasilimali watu, uchumi wa viwanda na utawala -- kama sehemu ya mpango wake kwa miaka mitano ijayo, inayolenga "kuzalisha na kuleta mageuzi katika mahitaji ya kila siku ya watu nchini."

Vipaumbele vitatolewa katika kuharakisha uchumi wa viwanda, kuboresha mazingira ya biashara, kutoa mafunzo kwa vijana na kuongeza nafasi za ajira ili kuboresha hali ya maisha, hasa kwa makundi ya watu walio hatarini zaidi, ameongeza.

Rajoelina pia ameapa kupambana na rushwa, akisisitiza kuweka kwake mkazo katika maadili ya uadilifu, udhati na uaminifu.

Rajoelina alikuwa rais wa nchi hiyo kuanzia Januari 2019 hadi Septemba 2023. Pia amewahi kuwa meya wa Mji Mkuu wa nchi hiyo, Antananarivo.

Andry Rajoelina, aliyechaguliwa tena kuwa Rais wa Madagascar, akitoa hotuba kwa taifa kwenye hafla ya kuapishwa kwake mjini Antananarivo, Madagascar, Desemba 16, 2023. (Picha na Sitraka Rajaonarison/Xinhua)

Andry Rajoelina (Kati), aliyechaguliwa tena kuwa Rais wa Madagascar, akikagua gwaride la heshima la jeshi kwenye hafla ya kuapishwa kwake mjini Antananarivo, Madagascar, Desemba 16, 2023. (Picha na Sitraka Rajaonarison/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha