

Lugha Nyingine
Mjumbe maalum wa Rais wa China ahudhuria hafla ya kuapishwa kwa Rais wa Madagascar Rajoelina
Rais wa Jamhuri ya Madagascar Andry Nirina Rajoelina akikutana na mjumbe maalum wa Rais Xi Jinping wa China na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Watu wa China Hu Chunhua mjini Antananarivo, Madagascar, Desemba 17, 2023. (Picha na Sitraka Rajaonarison/ Xinhua)
ANTANANARIVO - Kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Madagascar Andry Nirina Rajoelina, Hu Chunhua, Mjumbe Maalum wa Rais wa China Xi Jinping na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Watu wa China, amehudhuria hafla ya kuapishwa kwa Rais Rajoelina siku ya Jumamosi na baadaye kukutana naye siku ya Jumapili ambapo amemfikishia salamu za pongezi na za kumtakia kila la kheri kutoka kwa Rais Xi.
Hu amesema, China inatilia maanani sana maendeleo ya uhusiano kati ya China na Madagascar na iko tayari kushirikiana na Madagascar ili kuzidisha mabadilishano na ushirikiano katika nyanja mbalimbali, kuendelea kuungana mkono kithabiti katika masuala yanayohusu maslahi ya msingi na mambo yanayofuatiliwa zaidi na pande zote, na kuendeleza ushirika wao wa ushirikiano wa pande zote hadi ngazi mpya.
Kwa upande wake, Rais Rajoelina amemshukuru kwa dhati Rais wa China kwa kutuma mjumbe maalum kuhudhuria hafla hiyo ya kuapishwa kwake na kumuomba Hu kufikisha salamu zake za dhati na salamu za heri kwa Xi.
Amesema kuwa, Madagascar inathamini sana urafiki wa jadi na China na iko tayari kupanua ushirikiano na China katika masuala muhimu, kama vile kilimo, viwanda, nishati na rasilimali watu, ili kusukuma uhusiano kati ya nchi hizo mbili kufikia kiwango cha juu zaidi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma