

Lugha Nyingine
Ndege yaanguka Lamu, Kenya muda mfupi baada ya kushusha wanafunzi bora wa KCPE
(CRI Online) Desemba 19, 2023
Watu kumi, wakiwemo maafisa saba wa kijeshi, afisa wa polisi, rubani mkuu na rubani msaidizi, wamenusurika kufariki na kujeruhiwa Jumapili saa saba na nusu mchana wakati ndege ndogo aina ya Cessna ilipoanguka na kuwaka moto baada ya kugonga nguzo ya umeme na waya huko Kiunga, Kaunti ya Lamu kwenye mpaka wa Kenya na Somalia. Nyumba moja imeteketea katika ajali hiyo.
Naibu Kamishna wa Kaunti ya Lamu Mashariki George Kubai amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, akisema watu hao kumi walikuwa wakirejea Nairobi baada ya kuwashusha wanafunzi waliofanya vyema katika Mtihani wa Taifa wa Shule za Msingi wa Kenya (KCPE) wa Mwaka 2023 ambao walikuwa wanatoka ziara ya kielimu jijini Nairobi. Safari hiyo ilifadhiliwa na mbunge wa eneo hilo.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma