Wataalamu wa afya wahimiza uzalishaji wa chanjo barani Afrika

(CRI Online) Desemba 19, 2023

Wataalamu wa afya na viongozi wametoa wito wa kufanyika juhudi zaidi kuhimiza uzalishaji wa bidhaa za kimatibabu hasa chanjo barani Afrika, ili kutatua vipaumbele vya afya ya umma barani Afrika.

Wito huo umetolewa kwenye kongamano la ngazi ya juu lililowakutanisha mawaziri wa afya wa nchi za Afrika na wajumbe kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) na Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) mjini Kigali, kujadili mikakati ya kuimarisha uzalishaji wa bidhaa za kimatibabu barani Afrika kwa ajili ya kutatua vipaumbele vya afya ya umma barani humo.

Akiongea kwenye kongamano hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Africa CDC Jean Kaseya, amesema Africa CDC imeanzisha Ushirikiano wa Uzalishaji Chanjo kwa Afrika (PAVM) na imeweka mkakati wa miaka 20 unaolenga kuhakikisha asilimia 60 ya chanjo zinazohitajika barani Afrika zinazalishwa barani Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha