

Lugha Nyingine
Kenya yaadhimisha siku ya haki za makundi ya watu wachache ya Umoja wa Mataifa na kuhimiza kuwepo kwa usawa
Kenya imeungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha Siku ya Haki za Makundi ya Watu walio Wachache huku kukiwa na wito wa kuhimiza usawa miongoni mwa jamii za makundi ya watu walio wachache na wasiopewa umuhimu wanaoishi nchini humo.
Maadhimisho hayo yanayofanyika baada ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kupitisha tamko la haki za watu wa jamii ya makundi ya watu walio wachache wa kitaifa au kikabila, kidini na kilugha, yamekutanisha mashirika ya Umoja wa Mataifa, wanadiplomasia na maofisa wakuu wa serikali, kujadili njia za kuondoa ubaguzi dhidi ya makundi ya watu walio wachache.
Mkuu wa Mawaziri ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Diaspora wa Kenya Bw. Musalia Mudavadi, amewaambia wanahabari mjini Nairobi kuwa Kenya inaendelea kuwa na nia ya kuwasaidia watu wa makabila madogo kupitia uingiliaji kati unaolenga kuwawezesha kiuchumi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma