

Lugha Nyingine
Wataalamu watoa wito wa matumizi ya teknolojia ya Juncao kuhimiza kilimo endelevu barani Afrika
Wataalamu wanaohudhuria warsha kuhusu teknolojia ya Juncao mjini Addis Ababa, Ethiopia wametoa wito kwa juhudi za pamoja za matumizi ya teknolojia hiyo kuendeleza kilimo endelevu barani Afrika.
Warsha hiyo ya siku mbili imeandaliwa kwa pamoja na Ujumbe wa China kwenye Umoja wa Afrika (AU), Idara ya Umoja wa Mataifa ya Masuala ya Kiuchumi na Kijamii (UN-DESA), Kituo cha Taifa cha Utafiti na Uhandisi wa Teknolojia ya Juncao chini ya Chuo Kikuu cha Kilimo na Misitu cha Fujian nchini China (FAFU).
Kamishna wa AU anayeshughulikia kilimo, maendeleo ya vijijini, uchumi wa bluu na mazingira endelevu Bw. Joseph Sacko, ameeleza uungaji mkono mkubwa na utayari wa AU katika kushirikiana na China kwenye matumizi ya teknolojia ya Juncao kote barani Afrika.
Amesema teknolojia ya Juncao ni yenye gharama nafuu na itasaidia kufikia uhakika wa chakula na kupunguza umaskini miongoni mwa watu maskini vijijini. Teknolojia hiyo imethibitishwa kwenye uzalishaji wa uyoga na malisho ya mifugo, na inatarajiwa kuchangia katika kupambana na utapiamlo barani Afrika.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma