Rais Xi Jinping ampongeza Abdel-Fattah al-Sisi kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Misri

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 20, 2023

Beijing - Rais wa China Xi Jinping ametuma ujumbe wa pongezi kwa Abdel-Fattah al-Sisi siku ya Jumanne kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Misri, akisema kuwa China na Misri ni marafiki wazuri ambao wana mtazamo sawa na wenye kuaminiana, na ni washirika wazuri wanaofanya juhudi kwa ajili ya kupata maendeleo na ustawi kwa pamoja.

Amesema, katika miaka ya hivi karibuni uhusiano kati ya China na Misri umeimarika, ushirikiano wa kufuata hali halisi katika sekta mbalimbali umeleta matokeo yenye matunda, na urafiki kati ya watu wa pande hizo mbili umekuwa ukiongezeka siku hadi siku.

Rais Xi amesema anatilia maanani sana maendeleo ya uhusiano kati ya China na Misri, na angependa kushirikiana na Rais Sisi ili kuendelea kuungana mkono kithabiti, kuendeleza ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Nji Moja, kulinda kwa pamoja maslahi ya pamoja ya nchi zinazoendelea, na kuendelea kuinua uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Misri hadi ngazi za juu ili kuleta manufaa zaidi kwa watu wa pande mbili.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha