

Lugha Nyingine
China yakanusha kashfa za Bunge la Ulaya dhidi ya shule za bweni katika Mkoa wa Xizang
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Wang Wenbin amesema mashambulizi na kashfa za Bunge la Ulaya dhidi ya shule za bweni katika Mkoa unaojiendesha wa Xizang nchini China ni aina fulani ya ukiukaji wa haki ya elimu ya watoto, ambayo ni uharibifu wa hali ya haki za binadamu katika mkoa huo.
Msemaji Wang ameyasema hayo siku ya Jumanne kwenye mkutano na waandishi wa habari, wakati akijibu swali kwamba Bunge la Ulaya limepitisha azimio la kukosoa kitendo cha serikali ya China kulazimisha kuwabadili jadi zao watoto wa Kabila la Watibeti kupitia shule za bweni za Xizang, na kutoa wito kwa Umoja wa Ulaya na nchi wanachama wake kuchukua hatua.
"Kinachosemwa katika azimio husika la Bunge la Ulaya ni habari potofu," Wang amesema. "Inachafua taswira ya China na kuingilia masuala ya ndani ya China. Tunasikitika na tunapinga vikali hili."
Wang amesisitiza kuwa, katika Mkoa wa Xizang, haki na uhuru wa makabila yote, ikiwa ni pamoja na uhuru wa imani ya kidini na uhuru wa kutumia na kuendeleza lugha zao, zinalindwa kikamilifu.
"Hali za haki za binadamu huko Xizang ni bora kuliko hapo awali, kama ilivyoshuhudiwa na jumuiya ya kimataifa," amesema.
Amefafanua kuwa kwa upande wa Xizang, kutokana na watu kutawanyika sana, watoto hulazimika kusafiri umbali mrefu kufika shuleni, jambo ambalo ni la usumbufu mkubwa. Amesema kwamba kama shule zingejengwa katika kila sehemu wanayoishi wanafunzi, ingekuwa vigumu sana kuhakikisha kuna walimu wa kutosha na ubora wa ufundishaji katika kila shule.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma