

Lugha Nyingine
Mawaziri wakuu wa China na Russia waongoza kwa pamoja mkutano wa 28 kati ya wakuu wa serikali za China na Russia
![]() |
Waziri Mkuu wa China Li Qiang na Waziri Mkuu wa Shirikisho la Russia Mikhail Mishustin kwa pamoja wakiongoza mkutano wa 28 kati ya wakuu wa serikali za China na Russia kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Desemba 19, 2023. (Xinhua/Pang Xinglei) |
BEIJING - Waziri Mkuu wa China Li Qiang na Waziri Mkuu wa Russia Mikhail Mishustin wameongoza kwa pamoja mkutano wa 28 kati ya wakuu wa serikali za China na Russia siku ya Jumanne mjini Beijing akisema kwamba chini ya mwongozo wa kimkakati wa wakuu wa nchi hizo mbili, uhusiano kati ya China na Russia umeendelezwa kwenye kiwango cha juu, huku kukiwa na hali imara zaidi wa kuaminiana kisiasa, kuimarika kwa urafiki kati ya watu wa pande hizo mbili, ushirikiano thabiti wa kivitendo, na uratibu wa karibu wa kimataifa, na kuweka mfano mpya wa uhusiano kati ya nchi kubwa.
Amesema, China iko tayari kushirikiana na Russia kutumia fursa ya maadhimisho ya kutimia miaka 75 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia mwakani ili kutekeleza makubaliano muhimu yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili, kuendelea kuurithisha urafiki kati ya China na Russia kutoka kizazi hadi kizazi, na kusukuma maendeleo mapya na makubwa zaidi ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Kwa upande wake Mishustin ametuma salamu za rambirambi kwa China kutokana na tetemeko la ardhi lililoikumba Wilaya ya Jishishan katika Mkoa wa Gansu, Kaskazini Magharibi mwa China.
Amesema Russia iko tayari kushirikiana na China kutekeleza makubaliano muhimu yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili, kuimarisha ushirikiano katika nyanja za uchumi, biashara, nishati na uwekezaji, kuimarisha mabadilishano ya kitamaduni na kati ya watu, na kuimarisha mawasiliano na uratibu ndani ya mifumo ya kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa na BRICS.
Pande hizo mbili zimekubaliana kuwa, hivi sasa, China na Russia zimeweka mkazo zaidi katika maendeleo na ustawi. Kwamba, pande hizo mbili zinapaswa kuongeza vichocheo vya ndani vya kuendeleza uhusiano kati ya China na Russia, kupanua ushirikiano wa kibiashara na kilimo kati ya nchi hizo mbili, kuweka mazingira bora ya biashara kwa kampuni za upande mwingine kuwekeza katika nchi zao, kulinda kwa pamoja usalama wa nishati wa nchi hizo mbili, kuimarisha muunganisho, kuongeza mabadilishano ya wataalam na ushirikiano wa serikali za mitaa, na kuhakikisha usalama na uthabiti wa minyororo ya viwanda na ugavi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma