Ubalozi wa China waikabidhi Somalia dola za kimarekani zaidi ya milioni moja kusaidia waathirika wa mafuriko

(CRI Online) Desemba 20, 2023

Ubalozi wa China nchini Somalia umeikabidhi serikali ya Somalia msaada wa kibinadamu wenye thamani ya dola za kimarekani zaidi ya milioni moja kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni nchini humo.

Balozi wa China nchini Somalia Fei Shangchao amesema msaada huo unatarajiwa kuleta ahueni kwa waathirika hao. Kamishna wa shirika la usimamizi wa maafa la Somalia Bw. Mohamud Moallim Abdulle ameshukuru msaada huo kutoka China.

Takwimu zilizotolewa na serikali ya Somalia zinaonesha kuwa, mafuriko katika maeneo ya kusini na kati mwa nchi hiyo yamesababisha vifo vya watu zaidi ya mia moja na wengine milioni 1.7 kulazimika kuhama makazi yao.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha