Mwanariadha wa zamani wa Kenya afariki dunia wakati akimuokoa mbwa wa mwajiri wake

(CRI Online) Desemba 20, 2023

Mwanariadha wa zamani wa Kenya Josephat Kibet Ngetich amefariki majini alipokuwa akijaribu kumwokoa mbwa aliyeanguka kwa bahati mbaya majini kwenye bwawa siku ya Jumanne, wiki iliyopita katika makazi ya mwajiri wake nchini Mexico.

Familia yake huko Kenya iliarifiwa kuhusu kifo cha mpendwa wao Alhamisi, wiki iliyopita na kuzua taharuki kubwa katika kijiji cha Taabet, kata ya Chesoen, jimbo kibunge la Bomet ya Kati, kaunti ya Bomet.

Kifo chake kimeiacha familia yake katika mfadhaiko na haijulikani ni kwa nini aliamua kuhatarisha maisha yake ili kuokoa mbwa huyo.

Hata hivyo familia hiyo inasema haiwezi kukusanya Sh milioni tatu za Kenya zinazohitajika ili mwili urudishwe nyumbani.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha