

Lugha Nyingine
Zambia yakamata raia wa Uingereza akiwa na kilo 5.7 za cocaine
(CRI Online) Desemba 20, 2023
Idara ya kupambana na dawa za kulevya ya Zambia imemkamata raia mmoja wa Uingereza mwenye asili ya Tanzania mwenye umri wa miaka 64 akiwa na kilo 5.7 za dawa za kulevya aina ya cocaine.
Mshukiwa huyu amekamatwa jana Jumanne kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Simon Mwansa Kapwepwe mjini Ndola, akijaribu kuingia kwenye ndege ya kwenda Ujerumani.
Ofisa mahusiano wa Kamisheni ya Kupambana na Dawa za Kulevya (DEC) nchini Zambia, Bw. Mwenge Mulenga amesema mshukiwa huyo ambaye amewahi kutuhumiwa kwa uhalifu nchini Uingereza, alishukiwa kuwa na uhusiano na kundi moja la kimataifa la dawa za kulevya linalofanya shughuli nchini Tanzania na Ujerumani.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma