

Lugha Nyingine
DRC kufanya uchaguzi mkuu kukiwa na changamoto ya usalama na ugavi wa vifaa vya uchaguzi
Wapiga kura takriban milioni 44 wanapiga kura leo Jumatano nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo wa rais, wabunge wa taifa na wabunge wa majimbo huku kukiwa na changamoto ya usalama.
Kuna wagombea 26 kwenye nafasi ya urais walioandikishwa na Tume ya Uchaguzi ya DRC (CENI), wakiwemo Rais aliyeko madarakani sasa Felix Tshisekedi, Moise Katumbi, gavana wa zamani wa Jimbo la Katanga, Denis Mukwege, mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ya 2018, pamoja na Martin Fayulu, ambaye bado anajiona kuwa mshindi halali wa uchaguzi wa urais wa 2018.
Licha ya kuwepo kwa changamoto kuhusu vifaa vya uchaguzi tume ya uchaguzi ya nchi hiyo imesema uchaguzi utafanyika kama ilivyopangwa.
Habari zinasema Jumuiya ya Afrika Mashariki haitatuma timu ya waangalizi kwenye uchaguzi huo kutokana na mamlaka husika za DRC kutotuma mwaliko.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma