Rais Xi Jinping wa China asisitiza kuimarisha msingi wa kilimo na kuhimiza ustawishaji wa vijiji

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 21, 2023

Naibu Waziri Mkuu wa China Liu Guozhong, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, akihudhuria na kutoa hotuba kwenye mkutano wa Kamati kuu ya Chama kuhusu kazi za vijiji uliofanyika Jumanne na Jumatano mjini Beijing, China. (Xinhua/Yin Bogu)

Naibu Waziri Mkuu wa China Liu Guozhong, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, akihudhuria na kutoa hotuba kwenye mkutano wa Kamati kuu ya Chama kuhusu kazi za vijiji uliofanyika Jumanne na Jumatano mjini Beijing, China. (Xinhua/Yin Bogu)

BEIJING - Mkutano wa kila mwaka wa Kamati kuu ya Chama kuhusu kazi za vijiji umefanyika Beijing kuanzia Jumanne hadi Jumatano, ukiainisha vipaumbele vya kazi za vijiji katika Mwaka 2024, ambapo Rais Xi Jinping wa China ametoa maagizo muhimu kuhusu kazi za kilimo, vijiji na wakulima akisema katika Mwaka 2023, China imeshinda maafa na hali nyingine mbaya, imepata rekodi mpya katika pato la mazao ya nafaka, imehakikisha ongezeko la haraka la mapato ya wakulima, na kudumisha maafikiano na utulivu katika vijiji.

Rais Xi ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) amesema ili kuendeleza maendeleo ya mambo ya kisasa, China lazima ifanye juhudi zisizolegalega ili kuimarisha msingi wa sekta ya kilimo na kuhimiza ustawishaji wa vijiji kwa pande zote.

Amesema, ni lazima kuiga uzoefu wa Mpango wa Ustawishaji wa Kijani Vijijini, kufanya juhudi kwa kufuata hali halisi, kutekeleza sera mahsusi, kuchukua hatua madhubuti za kudumisha maendeleo, ili kufikia matokeo halisi na kuleta manufaa kwa wananchi.

Rais Xi amesisitiza kwamba usalama wa chakula lazima ulindwe kwa kuweka hali tulivu ya matumizi ya ekari za ardhi kwa ajili ya uzalishaji wa nafaka na kuongeza mavuno kwa kila ekari. Amesema ni lazima kuanzisha mfumo wa utoaji wa chakula wa aina mbalimbali, na kuboresha sifa ya mashamba ya upandaji wa nafaka.

Amesisitiza kwamba, ni lazima jitihada zifanyike kuhakikisha kazi nzuri ya kukarabati na kujenga upya baada ya maafa, kuimarisha uwezo wa kuzuia, kupunguza na kutoa msaada wakati wa maafa, na kuepuka kurejea katika hali ya umaskini kwa watu wengi.

Rais Xi pia amehimiza juhudi za kuimarisha maendeleo ya viwanda vijijini, ujenzi na utawala wa maeneo ya vijijini, na kujitahidi kupata maendeleo makubwa katika kuhimiza ustawishaji wa vijiji kwa pande zote.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha