

Lugha Nyingine
Mjumbe wa China asisitiza kusimamisha mapigano kama kipaumbele cha kwanza katika eneo la Ukanda wa Gaza
Picha hii iliyopigwa Desemba 19, 2023 ikionyesha mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Mashariki ya Kati, likiwemo suala la Palestina, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York. (Manuel Elias/Picha ya UN/ Xinhua)
UMOJA WA MATAIFA - Mjumbe wa China katika Umoja wa Mataifa, Zhang Jun amesema siku ya Jumanne kwamba kufikia usimamishaji wa vita katika Ukanda wa Gaza kwa sasa ni kipaumbele muhimu zaidi akisema jumuiya ya kimataifa, mara kwa mara na kwa wingi imekuwa ikitoa wito wa kusimamishwa kwa mapigano mara moja. "Hata hivyo Israel inaendelea na mashambulizi yake ya mabomu na makombora. Shule, hospitali, misikiti, makanisa ya Kikristo na kambi za wakimbizi zimekuwa zikilengwa mara kwa mara katika operesheni za kijeshi."
"Kwanza, kufikia usimamishaji wa mapigano unaendelea kuwa masharti makuu. Ni usimamishaji vita pekee ndiyo unaweza kuzuia maafa makubwa zaidi kwa raia, ikiwa ni pamoja na wale waliotekwa nyara. Ni usimamishaji vita pekee ambao unaweza kuzuia mgogoro wa kikanda kuenea na kushindwa kudhibitiwa. Na ni usimamishaji vita pekee unaoweza kuepusha matarajio ya suluhu ya kisiasa kuuliwa kabisa." Balozi Zhang amesema kwenye mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Mashariki ya Kati, likiwemo suala la Palestina.
"Hakuwezi kuwa na uhalali wa mashambulizi kama haya. Ni lazima ifahamike kuwa kusababisha vifo vya raia zaidi huko Gaza hakutafanikisha suluhu ya kuwaokoa mateka, wala hiyo haitaleta usalama zaidi kwa upande wowote," mjumbe huyo amesema.
"Tunaitaka Israel kubadili mara moja hatua yake na kuacha mashambulizi yake ya kijeshi ya kiholela dhidi ya watu wa Gaza," amesema.
Amesema kuwa shughuli za makazi ya walowezi wa kiyahudi zinakiuka sheria za kimataifa na azimio nambari 2334 la Baraza la Usalama na zinaendelea kumomonyoa msingi wa suluhu ya nchi mbili.
"Tunaitaka Israel, kama nchi inayoikalia Palestina kwa mabavu, ifuate wajibu wake chini ya sheria za kimataifa, kusitisha shughuli zote katika makazi ya walowezi, na kudhibiti kikamilifu ghasia za walowezi, ili kukomesha hali ya kutokujali," Zhang amesema.
Kuhusu suluhu ya kuunda nchi mbili, Zhang amesema kuwa mbinu hii lazima ihuishwe kwa nia mkubwa zaidi wa kisiasa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma