

Lugha Nyingine
Radi yaua watu wanne magharibi mwa Tanzania
(CRI Online) Desemba 21, 2023
Jeshi la Polisi nchini Tanzania limethibitisha kuwa watu wasiopungua wanne wameuawa na wengine wanane kujeruhiwa baada ya kupigwa radi Jumanne wiki hii huko wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, magharibi mwa nchi hiyo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo wa Kigoma Philemon Makungu amewaambia wanahabari kwamba watu hao walipigwa na radi hiyo na kufariki majira ya saa moja na nusu jioni ya Jumanne katika kijiji cha Buyezi wakiwa wamejikinga mvua katika mgahawa mmoja.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma