Rais wa Jamhuri ya Kongo azindua jingo la maduka lililojengwa na Kampuni ya China

(CRI Online) Desemba 21, 2023

Rais wa Jamhuri ya Kongo Denis Sassou Nguesso jana Jumatano mjini Brazzaville alizindua jengo jipya la maduka linaloaminika kuwa ni kubwa zaidi nchini humo.

Jengo hilo la maduka liitwalo “Brazza Mall”, liko kwenye eneo la Mpila na limejengwa na kampuni ya ujenzi ya China Jiangsu International kwenye eneo lililokuwa kambi ya jeshi iliyoharibiwa na milipuko mwezi Machi mwaka 2012.

Akiongea kwenye uzinduzi wa jengo hilo, meya wa Brazzaville, Dieudonne Bantsimba amesema jengo hilo litakuwa kituo cha kiuchumi na kitalii ambako shughuli za kibiashara zitafanyika.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha