China yakabidhi kituo kinachohamahama cha kufuatilia hali ya hewa kwa Botswana

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 22, 2023

Wang Xuefeng (wa pili kushoto), Balozi wa China nchini Botswana, na Grace Muzila (wa pili kulia), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mazingira na Utalii ya Botswana, wakisikiliza maelezo ya kujulisha hali ya kituo hiki baada ya hafla ya makabidhiano huko Gaborone, Botswana, Desemba 21 , 2023. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua)

GABORONE - Ubalozi wa China umekabidhi kituo kinachohamahama cha kufuatilia hali hewa chenye mfumo wa kupokea na kuchakata data za satelaiti nyingi kwa serikali ya Botswana huko Gaborone, Botswana, siku ya Alhamisi, kwa lengo la kusaidia kuboresha uwezo wa nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi.

Kituo hiki kitatoa msaada mkubwa kwa Botswana katika ufuatiliaji wa mazingira, uzalishaji wa kilimo na kuzuia hali hatari za tabianchi zilizokithiri, ili kusaidia Botswana kufikia malengo yake ya maendeleo endelevu ya mazingira, amesema Wang Xuefeng, Balozi wa China nchini Botswana kwenye hafla ya kukabidhi kituo hicho, huku akiongeza kuwa kituo hicho ni moja tu ya matunda ya mipango tisa chini ya Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika.

Ikiwa ni nchi kubwa zaidi inayoendelea duniani na inayowajibika, China siku zote imekuwa mtetezi na mtekelezaji madhubuti kwa vitendo wa ushirikiano wa Kusini na Kusini kuhusu mabadiliko ya tabianchi. Hadi sasa China imesaini makubaliano 48 ya ushirikiano na nchi 40 zinazoendelea, Balozi Wang amesema.

Kwa upande wake Grace Muzila, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mazingira na Utalii ya Botswana, amepokea kituo hicho kwa niaba ya serikali ya Botswana na kuishukuru serikali ya China kwa msaada wake wa kujitolea.

"Nchini Botswana, ukame wa mara kwa mara unazidisha uhaba wa maji na hivyo kuathiri vibaya afya na nguvu ya uzalishaji . Msaada huu utasaidia sana katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na kusaidia kuimarisha uwezo wetu wa kuweka maisha na mali za watu salama, kupunguza hatari ya maafa na kudumisha uchumi imara na unaotegemewa,” amesema.

Mnamo Novemba 2020, Wizara ya Ikolojia na Mazingira ya China na Wizara ya Mazingira na Utalii ya Botswana zilitia saini makubaliano ya maelewano (MoU) mjini Gaborone chini ya ushirikiano wa Kusini na Kusini kwa ajili ya kushughulikia mabadiliko ya tabianchi. Kwa mujibu wa MoU hiyo, serikali ya China ilikubali kuchangia mfumo wa kupokea na kuchakata data za satelaiti nyingi kwa Botswana, ili kusaidia kuboresha uwezo wa nchi hiyo kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Picha hii iliyopigwa Desemba 21, 2023 ikionyesha kituo kinachohamahama cha  kufuatilia hali ya hewa kilichokabidhiwa na Serikali ya China kwa Botswana mjini Gaborone, Botswana, Desemba 21, 2023. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha