

Lugha Nyingine
Mvutano unaoongezeka katika Bahari Nyekundu waathiri usafiri wa kimataifa wa meli, na kuzua wasiwasi wa mzozo wa Gaza kuenea
Watu wakikusanyika katika maandamano ya kuwaunga mkono Wapalestina huku kukiwa na mgogoro kati ya Palestina na Israel, mjini Sanaa, Yemen, Oktoba 20, 2023. (Picha na Mohammed Mohammed/Xinhua)
SANAA, Yemen - Waasi wa Houthi wa Yemen wanaongeza mashambulizi yao dhidi ya meli "zinazohusiana na Israeli" katika Bahari Nyekundu, wakitaka kulipiza kisasi kwa kampeni ya kijeshi ya Israeli huko Gaza ambapo mashambulizi hayo yanayoongezeka yamesababisha kampuni kubwa za meli na mafuta kusimamisha usafiri kupitia njia hiyo muhimu ya biashara, na kuzua wasiwasi kuhusu athari zinazoweza kutokea za kiuchumi duniani. Katika kukabiliana na hali hiyo, Marekani na nchi nyingine kadhaa zinaunda muungano mpya wa kulinda meli zinazopita Bahari Nyekundu.
Hata hivyo, kuongezeka kwa uwepo wa kijeshi katika Bahari Nyekundu, kama wachambuzi wanavyosema, kunaweza kuchochea uhasama mkubwa, na hivyo kuongeza wasiwasi kuhusu mgogoro kati ya Israel na Palestina kuenea katika eneo hilo.
Kuongezeka kwa mvutano
Katika muda wa wiki nne zilizopita, kundi la wanamgambo wa Houthi lenye makazi yake nchini Yemen, wameshambulia au kukamata meli za kibiashara mara 12 na bado wanawashikilia mateka 25 ambao ni wafanyakazi wa meli ya kibiashara ya Galaxy Leader nchini Yemen.
Wakati wa ziara yake mpya ya Mashariki ya Kati, Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin alitangaza Jumanne huko Bahrain kwamba Marekani inajenga muungano mpya wa kimataifa unaojumuisha nchi za Uingereza, Bahrain, Canada, Ufaransa, Italia, Uholanzi, Norway, Shelisheli na Hispania ili kuzilinda zinazopita Bahari Nyekundu.
Kwenye hotuba ya televisheni siku ya Jumatano, kiongozi wa Houthi Abdulmalik al-Houthi alisema, "Kama Marekani inatulenga, basi tutalipiza kisasi kwa kulenga meli za kivita za Marekani na maslahi yale katika eneo hili kwa makombora, droni na operesheni zetu za kijeshi."
Kuvurugika kwa usafiri
Wachambuzi wanasema kuongezeka kwa mvutano kwenye Bahari Nyekundu kunaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa biashara ya baharini na mnyororo wa ugavi duniani.
Salam Al-Asbahi, jenerali mstaafu wa vikosi vya serikali ya Yemen, anaonya kwamba kundi la Houthi linaweza kuvuruga ukanda wa Mfereji wa Suez – Bahari Nyekundu, ambao unashughulikia asilimia takriban 12 ya biashara ya Dunia.
Mgogoro kuenea
Kutumwa kwa vikosi hivyo vya muungano wa kijeshi vinavyoongozwa na Marekani katika Bahari Nyekundu kumeongeza wasiwasi juu ya uwezekano wa kuchochewa zaidi kwa mgogoro kati ya Israeli na Palestina na kuenea kwenye njia hiyo muhimu ya maji.
"Kuwepo kwa meli za kivita za Marekani pamoja na maslahi ya Israel kunaongeza uwezekano wa makabiliano yasiyotarajiwa na vikosi vya Houthi," amesema Al-Asbahi.
Boti ya makombora ya Jeshi la Majini la Israeli ikionekana katika eneo la Bahari Nyekundu Novemba 1, 2023. (Vikosi vya Ulinzi vya Israel/ Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma