

Lugha Nyingine
Taasisi ya tatu ya Confucius yafunguliwa nchini Ghana
![]() |
Wageni wakihudhuria hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Kwame Nkrumah mjini Kumasi, Ghana, Desemba 19, 2023. (Picha na Seth/Xinhua) |
ACCRA - Taasisi ya tatu ya Confucius nchini Ghana ambayo imeanzishwa kwa pamoja na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Kwame Nkrumah cha Ghana (KNUST) na Chuo Kikuu cha Teknolojia ya Magari cha Hubei cha China imefunguliwa rasmi siku ya Jumanne huko Kumasi, mji wa pili kwa ukubwa wake nchini Ghana, ili kuwezesha wanafunzi wenyeji kupata urahisi wa kujifunza lugha na utamaduni wa Kichina.
Kuanzishwa kwa Taasisi ya tatu ya Confucius nchini Ghana ambayo ni ya tatu ya aina yake kufuatia mbili za awali katika Chuo Kikuu cha Ghana na Chuo Kikuu cha Cape Coast mtawalia, kunaashiria ushirikiano wa pande zote katika elimu, kuhakikisha wahitimu wana uwezo kamili ya kitaaluma na kujitayarisha vya kutosha ili kukabiliana na changamoto za Dunia inayoendelea kubadilika, amesema Rita Akosua Dickson, Naibu Mkuu wa KNUST kwenye hafla ya uzinduzi.
"Taasisi ya Confucius itachukua jukumu muhimu katika kuwezesha KNUST kuwa na sehemu ya mfano ya nje ya nchi kwa masomo ya lugha ya Kichina za shahada ya kwanza na kujifunza lugha ya Kichina katika kanda za kati na kaskazini mwa Ghana," amesema.
Zhang Wenxue, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Teknolojia ya Magari cha Hubei, amesema Taasisi hiyo mpya ya Confucius itatumika kama jukwaa jingine la kuendeleza mabadilishano ya kitamaduni na kuimarisha urafiki kati ya nchi hizo mbili.
Tang Hong, Mkuu wa Shirikisho la Wachina wanaoishi Ghana, amesema wahitimu wa Ghana wenye ujuzi wa Lugha ya Kichina wanakaribishwa zaidi katika soko la kazi la nchini humo katika kipindi ambacho ushirikiano kati ya China na Ghana ukiendelea.
"Wafanyabiashara wengi zaidi wa Ghana wameanza kuwasiliana na washirika wao wa China kwa lugha ya Kichina. Nina imani kwamba kupitia mabadilishano na kujifunza zaidi kutoka kila upande, kizazi kipya kitakuwa nguvu mpya ya kuhamasisha maendeleo ya pamoja kati ya China na Ghana," Tang ameongeza.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma