

Lugha Nyingine
Guinea yatangaza siku tatu za maombolezo kufuatia ajali ya moto katika ghala la mafuta
(CRI Online) Desemba 22, 2023
Rais wa mpito wa Guinea Kanali Mamadi Doumbouya, ametangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa, kufuatia ajali ya moto iliyotokea katika ghala kubwa la mafuta usiku wa Jumapili mjini Conakry, na kusababisha vifo vya watu 18 na wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa.
Akihutubia taifa kwa njia ya televisheni, Rais Doumbouya ametangaza kuwa wakati wote wa kipindi hicho cha maombolezo ya kitaifa, bendera ya Guinea itapepea nusu mlingoti kote nchini humo na katika ofisi na balozi zake nje ya nchi.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma