

Lugha Nyingine
Mkuu wa jeshi la Sudan akataa makubaliano ya amani bila kuondoka kwa vikosi vya wanamgambo
(CRI Online) Desemba 22, 2023
Mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah Al-Burhan amesema jeshi lake halitasaini makubaliano yoyote ya amani yasiyohusisha kuondoka kwa Kikosi cha Mwitikio wa Haraka (RSF) kutoka kwenye miundombinu ya umma na nyumba za raia.
Bw. Al-Burhan ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza la Utawala wa Mpito la Sudan, ametoa kauli hiyo jana Alhamisi alipohutubia maofisa na askari katika jimbo la mashariki la Red Sea.
Bw. Al-Burhan amesema makubaliano yoyote yanatakiwa kuhusisha usimamishaji vita na kuondoka kwa waasi kutoka kwenye miundombinu ya umma, hospitali na nyumba za raia, akiongeza kuwa Jeshi la Sudan litaendelea na mapambano mpaka kuwashinda “wanamgambo waasi”.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma