

Lugha Nyingine
Usafirishaji wa shehena kupitia reli ya SGR nchini Kenya kwa mwaka 2023 watarajiwa kuimarika
Ripoti iliyotolewa Alhamisi wiki hii na Shirika la Reli la Kenya (KRC), imesema huduma ya usafirishaji kwa njia ya reli ya SGR nchini Kenya imerekodi ongezeko la asilimia 8 ya shehena katika miezi tisa ya kwanza ya mwaka huu, huku matumizi ya reli hiyo yakitarajiwa kushika kasi mwishoni mwa mwaka.
Reli hiyo iliyojengwa na China imesafirisha tani milioni 4.91 za mizigo kati ya Nairobi na Mombasa katika kipindi hicho, ikiwa ni ongezeko la kutoka tani milioni 4.55 za mizigo katika kipindi kama hicho mwaka jana. Idadi ya abiria waliotumia huduma ya usafiri ya SGR pia iliongezeka katika kipindi hicho kutoka abiria milioni 1.74 hadi milioni 1.95.
Shirika la Maendeleo ya Chai la Kenya (KTDA) pia limetoa taarifa ikisema reli hiyo imesafirisha mbolea zenye uzito wa tani zaidi ya elfu 45 za ujazo kwa wakulima wadogo wadogo wa chai, na kusema usafirishaji wa mbolea kwa reli hiyo unahakikisha ufanisi, kasi, usalama na kupunguza gharama.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma