Umoja wa Mataifa wapitisha azimio la kuifanya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China kuwa siku ya mapumziko ya Umoja wa Mataifa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 25, 2023

Tarehe 22, Desemba, mkutano wa Baraza Kuu la 78 la Umoja wa Mataifa (UN) ulipitisha azimio kwa kauli moja la kuifanya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China kuwa siku ya mapumziko ya Umoja wa Mataifa.

Kaimu mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Dai Bing alisema baada ya kupitishwa kwa azimio hilo kuwa, Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China imekuwa siku rasmi ya mapumziko ya Umoja wa Mataifa, hii imeonesha nguvu ya uenezi na ushawishi wa ustaarabu wa Taifa la China, na utahimiza kwa nguvu mawasiliano na kufundishana kati ya ustaarabu wa aina mbalimbali duniani na kuonesha dhana ya Umoja wa Mataifa kuhusu thamani ya utamaduni ulio wa pande nyingi na jumuishi.

Tovuti ya Umoja wa Mataifa imedhihirisha kuwa, kutokana na kupitishwa kwa azimio jipya la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Mwaka Mpya wa Jadi wa China kwa kalenda ya kilimo ya China unatazamiwa kuwa siku ya nane ya mapumziko ya Umoja wa Mataifa. Makao makuu ya Umoja wa Mataifa na mashirika yake yaliyoko sehemu mbalimbali yataepuka kufanya mkutano katika siku hiyo kila mwaka.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha